Bunge Marathon 2026 Mbio za Kihistoria-Sanga

GEORGE MARATO TV
0


MWENYEKITI wa Bunge Bonanza, Festo Sanga, amesema mashindano ya Bunge Marathon 2026 yanatarajiwa kuwa ya kipekee mwaka huu, yakilenga kuvunja rekodi na kuibua ushindani wa hali ya juu zaidi nchini.

Ameeleza kuwa tukio hilo litafanyika rasmi tarehe 18 Mei 2026, likiwa limeboreshwa kwa kiwango kikubwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa itakayorahisisha usimamizi wa mbio na kuhakikisha matokeo yanakuwa sahihi na ya kuaminika.



Sanga amesisitiza kuwa moja ya mambo yanayovutia zaidi ni ushiriki wa wazi kwa kila mtu, akibainisha kuwa mashindano hayo hayana mipaka ya uzoefu,hivyo kuwapa nafasi wanariadha wa kitaalamu na wananchi wa kawaida kushiriki na kuonesha uwezo wao.

Ameongeza kuwa matarajio ni kuona idadi kubwa ya washiriki ikiongezeka mwaka huu, huku Bunge Marathon 2026 ikilenga kuweka historia mpya na kuendelea kuhamasisha afya, mshikamano na ari ya ushindani miongoni mwa Watanzania.

"Maandalizi ya mbio za Marathon ya Wabunge yanayoandaliwa kwa mara ya kwanza yamekamilika, huku tukio hilo likitarajiwa kufanyika Aprili 18 mjini Dodoma". Amesema 

"Mbio hizo zitaanzia katika eneo maalum la kuanzia na kumalizikia katika Viwanja vya Jamhuri, ambapo waandaaji wameweka miundombinu rafiki ikiwemo vituo vya usajili, mahema na huduma muhimu kwa washiriki wote". Ameongeza 

Aid ha,Sanga Amesema Kwa waliopo Dar es Salaam, vituo maalum vimeandaliwa kwa ajili ya usajili na uchukuaji wa vifaa, huku walioko Dodoma wakihimizwa kufika Ofisi za Bunge kujisajili na kukamilisha taratibu zote muhimu.

"Marathon hii inalenga kuhamasisha mtindo bora wa maisha, kuimarisha afya za wananchi na kuunga mkono juhudi za Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kukuza sekta ya michezo nchini". Amesisitiza 

Kadhalika, amesema Washiriki watapata medali za viwango vya juu zenye nembo ya Bunge kwa umbali wa kilomita 5, 10 na 21, huku washindi wakitunukiwa medali maalum za ushindi zilizotengenezwa kwa ubora wa kipekee ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla.

"Tukio hili la kipekee linawakutanisha wabunge na wananchi kwa pamoja, likiwa jukwaa la kuimarisha mshikamano, mahusiano na uzalendo". Amesema

"Wananchi wote wananchi wote mnakaribishwa kushiriki katika marathon hii muhimu kwa afya na maendeleo ya Taifa". Amesisitiza

Naye Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, John Steven Akhwari, amesema Bunge Marathon kwa sasa imefikia hadhi ya kimataifa na kwamba nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na duniani zimepokea mialiko na kuthibitisha kushiriki. Naye, Mkurugenzi 

Kwa upande wake Mtendaji wa Kampuni ya Silent Ocean, Mohamed Soloka, ambao ndio wadhamini wakuu wa Bunge Marathon amesema maandalizi yote muhimu yamekamilika kupitia ushirikiano mzuri na kamati ya maandalizi.

Maandalizi ya Bunge Marathon Kwa mwaka huu 2026 yamekamilika kwa asilimia 100 huku mpaka sasa idadi ya waliojisajili imefikia zaidi ya watu 4200.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top