Waziri wa Ulinzi na Jeshi La Kujenga Taifa Mhe,Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho Amemtembelea na Kumjulia Hali Jenerali Mirisho Sarakikya

GEORGE MARATO TV
0


Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Mheshimiwa Rhimo Simeon Nyansaho (Mb) Leo Novemba 23, 2025 amemtembelea mkuu wa Majeshi wa mstaafu wa kwanza Mstaafu , jenerali Mirisho sarakikya nyumbani kwake Arumeru jijini Arusha kumsalimia na kumjulia hali 

Mheshimiwa Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho amefanya ziara hiyo ya kwanza kwa jenerali Mirisho sarakikya tangu ateuliwe kuwa waziri wa Ulinzi na JKT na mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mhe,Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Mhe,Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho amemueleza Jenerali Mirisho sarakikya kuwa wizara inatambua na kuthamini mchango wa wakuu wa Majeshi wastaafu jeshini na serikalini kwa ujumla , akimuahidi jenerali mstaafu sarakikya ushirikiano wake

Upande wake jenerali Mirisho sarakikya amemshukuru waziri wa Ulinzi kwa kumtembelea na kumjulia hali na akamshukuru mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua Mhe, Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho, kuwa waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa. 




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top