Na Ada Ouko, GMTV Musoma.
WAKAZI wa Manispaa ya Musoma wameaswa kuhamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuachana na matumizi ya nishati isiyo safi kutokana na athari zake kwa binadamu na mazingira.
Wito huo umetolewa Agosti 17,2025 na Afisa Uhusiano na huduma(TANESCO ) mkoa wa Mara Joyce Makori wakati akitoa elimu juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwenye uwanja wa Mara sekondari kwenye mkesha wa mbio za Mwenge wa uhuru.
" Tumekuja hapa na majiko ya umeme na kufanya mapishi mubashara kwa wananchi kwa kuonyesha kwa mfano ni jinsi gani ukitumia majiko ya umeme unaweza ukatumia umeme kidogo na ukapika chakula vizuri kwa gharama nafu pia kukaokoa muda"
Amesema TANESCO mkoa wa Mara ina muunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Hassan na kwamba majiko ya umeme yamefanyiwa utafiti na wataalam wa Tanesco.
"Watafiti wetu wa Tanesco wamegundua kuwa unapopika nyama au maharage kilo moja kwa kutumia nishati ya umeme kwa majiko haya unaseti kwa dakika 40 tu unatumia unit 0.9 ambayo ni sawa na shilingi 310 jambo ambalo kwa matumizi ya kuni au mkaa si rahisi kununua mkaa wa 310, au kuni za 310 kwa ajili ya kupikia wala hakuna mkaa wa 310" Amesema Joyce.
Aidha mbali na wito huo amewaasa wateja wao na wananchi kwa ujumla kulinda na kuhifadhi miundombinu ya umeme ili waweze kupata huduma hiyo kwa uhakika sambamba na hilo aliwataka kulipa madeni ili huduma itolewe kwao kwa uendelevu.










