Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Viongozi mkoani Tanga wametakiwa kuiga mfano kutoka Kwa mwenyekiti wa CCM Mkoa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa Rajabu Abdarahman ambapo hujali,kuasidi na kusikiliza bila ubaguzi wa aina yoyote.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyinga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM Mabala Mlolwa wakati wa dua ya kuwaombea waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika wilayani Pangani Kijiji Cha Stahabu pwani na kuwakutanisaha wanazuoni kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Tanga.
Aidha Mlolwa aliongeza kuwa ili kupata mafanikio katika uongozi ni lazima kuwa mtu wa watu na ukiweka maslahi binafsi mbele, ubaguzi ama majivuno ni ngumu kufanikiwa.
"Nimpongeze ndugu yangu Rajabu kwa jambo hili kwani sio jambo dogo kuwakutanisaha wananchi kutoka wilaya zote za mkoa,kweli hapa umeweza kudhihirisha kuwa wewe ni kiongozi wa mkoa na unayejali", Mlolwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti Rajabu amefanikiwa kuwashika mkono vijana wa Ahlu zaaman wanaotoa burudani kwa mkumsifu mtume. Muhammad (SAW) Kwa kuwapatia vifaa vya kisasa vya muziki na usfiri ili kurahisisha utendaji kazi wao.

Comments
Post a Comment