Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Buriani afungua milango Kwa wadau wanaopenda maendeleo kuchangia ujenzi wa kituo cha tiba ya moyo KCMC.
Ametoa Rai hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake akiwaalika wadau katika hafla ya chakula Cha jioni kitachofanyika katika hoteli ya Tanga beach resort,wadau hao ni wafanya biashara,wawekezaji na sekta ya afya.
Balozi Batilda amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho Hadi kukamilika kwake utagharimu kiasi Cha shilingi bilioni 25 na mpaka sasa zilizopatikana ni shilingi bilioni 22 na kufemea shilingi bilioni 3.
"Ujenzi wa kituo hicho ni neema Kwa wagonjwa wa ukanda huu wa kaskazini kwani kumekuwa na wangonjwa wengi wanaoshindwa kufika muhimbili kupatiwa matibabu kutokana na hali,hivyo basi niwaombe wafanya biashara na wadau wengine kuchangia ili kisaidia upatikanaji wa vifaa tiba kwani pesa iliyopatikana ambayo shilingi bilioni 22 inatarajiwa kukamilisha jengo lote na zinahitajika bilioni 3 Kwaajili ya vifaa tiba na pia unapotoa unakuwa umejiwekezea kwa mungu kwani hii ni sadaka inayoendelea",Balozi Batilda.
Kwa upande wake mratibu wa maradi wa ujenzi wa kituo hicho Cha tiba ya moyo KCMC Dr. Emanuel Bianchi amesema kuwa ujenzi huo mpaka sasa umefikia 40% na endapo kitakamilika kisaidia kutapunguza rufaa kutoka KCMC kwenda JKCI.



Comments
Post a Comment