Na Godfrey Marwa, Serengeti
Mwenyekiti wa baraza la madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Ayubu Mwita Makuruma amebainisha kuwa uwanja wa Kimataiafa wa Serengeti umepata mwafaka kwa msaada wa Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tayari serikali imeanza hatua mbalimbali rasmi kuanza utekelezaji wa mradi huo uliosubiliwa kwa miaka mingi ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na kijamii kupitia utalii
Aliyasema hayo katika kikao cha baraza hilo cha robo ya tatu kuanzia Januari hadi Machi, 2026,kilichofanyika jana Mei,20,2026, kupokea taarifa za maendeleo kutoka katika kamati za Halmashauri hiyo pamoja na taasisi za serikali na mashirika.
"Suala la uwanja wa ndege limepata mwafaka kwa msaada wa Dkt.Samia Suluhu Hassan,mbunge peleka salaam,tunafurahi mambo yanavyoendelea hivi karibuni timu maalu inakuja Serengeti kuhakikisha ujenzi unaenda kuanza,,
Kwa upande mwingine madiwani wa baraza hilo wameshiriki hafla ya kupokea mgawanyo wa fedha milioni 88,za mfuko wa jimbo kwa kukabidhiwa na Mary Daniel (mbunge),hundi ya milioni 25, kukamilishaji Zahanati ya Kisaka,madawati yenye thamani ya milioni 2,kwa ajili ya shule ya msingi Kambarage,saruji 2597 kwa kata 30,huku sehemu mifuko ya saruji 500,ikiwa ni sehemu ya msaada kutoka Nyansaho Foundation.
"Mary ameanza vizuri,historia itamkumbuka umeleta simenti, madawati milioni 25 kukamilisha Zahanati ya Kisala,alise Ayubu Makuruma na kuongeza
"Waheshimiwa madiwani mwenzetu muda umeanza kumtetea na sisi tunapaswa kuwa hapo,Vifaa hivi viende vikafanye kazi ilivyokusudiwa,
Naye Mbunge,Mary Daniel ambaye ni mjumbe wa baraza hilo la madiwanin alitumia fursa hiyo kuwataka madiwani kuhakikisha wanasimamia vifaa hivyo ili vitumike kama ilivyokusudiwa katika kuboresha kukamilisha majengo katika kata zao.





Comments
Post a Comment