Uharibifu huo pia mkubwa umehusisha miundo mbinu mingine ikiwemo ya shirika la umeme nchini Tanesco na vituo vya kuuzia nishati ya mafuta.
Kwa mujibu wa mashuhuda mvua hiyo ikiwa na kimbunga kikali imenyesha majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo machi 24 mwaka 2025.
Hadi sasa Serikali haijatoa taarifa rasmi ya madhara ambayo yamesababushwa na kimbunga hicho ikiwemo mvua hiyi kubwa ambayo imeelezwa kuwa haijawahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.
Mbunge wa Musoma mjini mh Vedastus Mathayo akizungumza kwa njia ya simu ameonesha kusikitishwa na tukio hilo kubwa na kutoa Pole kwa wananchi,taasisi na wafanyabiashara ambao wameathiriwa na janga hilo kubwa.
Maeneo mengi yaliyoathitiwa na janga hilo ni mitaa katibu yote ya katikati ya mji wa Musoma.










Comments
Post a Comment