Leo na mimi nataka ku share kidogo umuhimu wa VETA na kwanini uende VETA. VETA ni muendelezo wa tranformation ya masuala ya Ufundi stadi, kwa faida ya GEN-Z ni kwamba awali ilianza National Vocational Training Centre ( NVTC) ikaenda tena kuwa National Vocational Training Division ( NVTD) kabla ya kuwa VETA.
Binafsi sikusoma Form 5&6, baada ya kumaliza Form 4 nikajiunga na NVTC kusomea ufundi Umeme wa majumbani (Electrical Installation) na kupata cheti cha Daraja la III.
Stadi (skills) nilizopata zilinisaidia sana wakati huo pamoja na wenzangu kupata deals za kufunga umeme kwenye nyumba za watu ikiwemo pia maghorofa. Niliutumia ujuzi huo kwa kujipatia kipato kabla sija develop interest kuwa journalist. Nikaenda chuo na kufanikiwa kuhitimu shahada mbili za mawasiliano ya Umma (masters degree in MassCommunication), faida niliyonayo sasa ni kwamba hakuna fundi anayeweza kunidanganya kuhusu masuala ya umeme wa majumbani aidha ninaweza pia kumpa ushauri rafiki yangu ama yeyote kuhusu namna bora ya kufunga umeme nyumbani kwake.
*Umuhimu wa VETA* stadi unazopata zinakukusaidia hata ukiwa na maarifa (knowledge) ya kitu kingine.
Mfano halisi Mimi ni Mtu wa Mawasiliano lakini faida niliyopata VETA, ni kwamba hakuna fundi atanidanganya kuhusu Installation kwa mfano wire za 1.5mm na 2.5 mm zina matumizi gani ndani ya nyumba, kwanini Umeme una trip, taa zote iwe za incandescent, ama bulb, holder's, nafunga mwenyewe, najua ku trace short imetokea wapi na kwa vipi naweza kussolve, najua aina gani ya cable za kutumia kwa matumizi husika. Suala la back up sipigwi, najua kujumlisha watts za vifaa vyangu na ninamwambia muuzaji anipatie back up ya watts ninayoitaka kwa matumizi yangu.. Hiyo ni miongoni mwa faida za kuwa na stadi kutoka VETA.
Faida ya kupitia VETA kiuchumi, unaweza kujiajiri ama kuajiriwa kutokana na ujuzi. Kwenye ushindani wa ajira, Form Four mwenye stadi ya VETA hawezi kuwa sawa na Form 6 fresh from school ama Mwenye diploma linapokuja suala la ujuzi kwenye eneo husika.
Kuwa na stadi katika eneo fulani mfano Ujenzi huku ukiwa umeajiriwa katika taaluma nyingine, unaweza kupata tenda na ukawapa vibarua wafanye kazi huku wewe ukisimamia kutokea kazini kwako.
NB: lengo langu ni kushea umuhimu wa VETA na faida zake kuongeza kipato.
Fredy Mwanjala
HPRU- TRC.

Comments
Post a Comment