Mbunge wa Jimbo la Katavi Thomas Kampala ameonya kuhusu athari anazodai zinaweza kujitokeza katika jamii kutokana na kile alichokitaja kuwa kudhoofika kwa misingi ya malezi na maadili, akisema baada ya miaka 20 huenda kukawa na changamoto ya wanawake kupata wanaume wa kuanzisha nao familia. Akizungumza Novemba 6, 2026, katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mbunge huyo amesema jamii inapaswa kushirikiana kurejesha misingi ya malezi iliyoachwa nyuma, huku akitaka Serikali kupitia wizara zinazohusika kuchukua hatua kuhusu masuala ya ushoga na usagaji. Amesema mjadala aliougusia katika Bunge hili ulikuwa mfupi, lakini amedhamiria kufungua mjadala mpana zaidi katika Bunge lijalo ili kujadili changamoto hizo na namna ya kukabiliana nazo. Katika hatua nyingine, ameeleza kutounga mkono kufutwa kwa adhabu za viboko mashuleni, akipendekeza zirejeshwe kama sehemu ya kuimarisha nidhamu na malezi ya watoto. Aidha, amewataka wazazi na walezi kutambua umuhimu wa kuwalea watoto wa kiume na wa kike k...
Marato tv - Sauti ya Jamii