Skip to main content

Posts

Showing posts from March 8, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Akagua Ujenzi wa Soko la Kisasa la Mazao Kanondo-Rukwa

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Machi 8, 2026 ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Soko la Kisasa la Mazao Kanondo lililopo Sumbawanga mkoani Rukwa. Ujenzi wa soko hilo unatekelezwa kupitia Mradi wa TACTIC kwa gharama ya shilingi bilioni 7.3, na hadi sasa umefikia asilimia 82 ya utekelezaji. Soko hilo linatarajiwa kuwa kitovu muhimu cha biashara ya mazao, likiwaunganisha wakulima, wanunuzi wakubwa, wasafirishaji na wawekezaji, hatua itakayopanua mtandao wa biashara na kuongeza thamani ya mazao ya wakulima wa Rukwa na maeneo jirani.

Balozi Matinyi Afuturu na Diaspora wa Sweden na Kuwaaga

Mheshimiwa Balozi Mobhare Matinyi akitoa nasaha zake na kuwaaga Watanzania waishio nchini Sweden wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Ubalozi jijini Stockholm, Jumamosi, tarehe 7 Machi, 2026.

Dkt. Mwigulu Aagiza Takukuru Kuchunguza Fedha za Miradi Rukwa

_Akemea ucheleweshaji wa miradi, asema fedha za maendeleo si siri_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa kina kuhusu matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Rukwa kufuatia taarifa za kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi hiyo. Ametoa agizo hilo leo Jumapili (Machi 8, 2026) wakati akizungumza na mamia ya wananchi wa Laela mkoani Rukwa baada ya kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika eneo hilo. Dkt. Mwigulu amesema Serikali haitavumilia kuona miradi ya maendeleo ikicheleweshwa wakati fedha zake tayari zimetolewa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.lll  “Kamanda wa TAKUKURU nifanyie uchunguzi wa kina, senti mpaka senti, yeyote aliyehusika kwenye hii fedha hapa nipe taarifa hiyo ili niweze kufanya maamuzi,” amesema. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameonesha kutoridhishwa na kuchelewa kwa utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo ikiwemo uj...

Waziri Mkuu Akagua Ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Machi 08, 2026 amekagua maendeleo ya ukarabati na uboreshaji wa Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga uliopo mkoani Rukwa. Mradi huo ulianza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 kwa gharama ya shilingi bilioni 60.1 na hadi sasa umefikia asilimia 96 ya utekelezaji. Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Dkt. Mwigulu amewapongeza wananchi wa Rukwa kwa kupata uwanja wa ndege wa kisasa kwa kuwa maendeleo hayo yanaonesha mabadiliko makubwa ya mkoa huo. Amesema kuwa kwasasa Rukwa siyo ile ya zamani bali ni Rukwa ya kisasa na ya viwango, inayokwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya taifa. Aidha, amesema miradi ya aina hiyo ndiyo mafanikio ambayo Serikali ya Awamu ya Sita inajivunia kwa kuwekeza katika miradi ya maendeleo yenye tija na inayoacha alama kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Ukarabati na upanuzi wa uwanja huo unatarajiwa kuimarisha huduma za usafiri wa anga katika Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini pamoja na kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii. Mheshi...