Skip to main content

Posts

Showing posts from July 26, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Awasili Ruangwa Kwa Ajili ya Harambee ya Ujenzi wa Kanisa na Jubilei

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Wolfgang Pisa ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, alipowasili wilayani Ruangwa kwa ajili ya Harambee ya Ujenzi wa Kanisa na maandalizi ya Jubilei ya miaka 25 ya Upadre wa Mhashamu Askofu Wolfgang na miaka 50 ya Upadre wa Mhashamu Askofu Bruno Ngonyani, ambaye ni Aksofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki Lindi. Ujenzi wa Kanisa hilo unategemea kugharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 6.6

Waziri Mkuu Akutana na Kuzungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ndanda

WAZIRI Mkuu Mh Kassim Majaliwa amekutana na kuzungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ndanda iliyopo Wilaya ya Masasi na Shule ya Msingi Nachingwea iliyopo Wilaya ya Nachingwea. Wanafunzi hao ambao wako wilayani Nachingwea kwa ajili ya ziara ya kitaaluma ikihusisha ufanyaji wa mitihani ya kujipima ya ujirani mwema. Wakiwa uwanja wa ndege wa Nachingwea kwa ajili ya Kujifunza majukumu ya uwanja wa ndege,wanafunzi hao wameta fursa hiyo  ya kumpokea na kuzungumza na waziri mkuu katika maeneo hayo. Waziri mkuu Majaliwa amewasili Wilayani Nachingwea akielekea wilayani Ruangwa ambapo atakuwa mgeni Rasmi katika  harambee ya Kanisa Katoliki jimbo la Lindi. Harambee hiyo kwa ajili ya Maandalizi ya Jubilei na ujenzi wa kanisa jipya la jimbo katoliki Lindi inayafanyika leo Julai 27, 2024 wilayani Ruangwa.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Kanda ya Ziwa Watoa Tamko Matukio ya Utekaji na Mauaji

Na Robinson Wangaso – Mwanza. Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania THRDC kanda ya Ziwa, umesema  matukio ya utekwaji na kuibiwa kwa watoto katika mikoa ya Kanda ya Ziwa  kwa  mwaka 2023/2024  yakiwemo matukio ya mauaji ya watu wenye Ualibino yaliyoripotiwa ni 73 jambo ambalo linapaswa kuchukuliwa hstua na kudhibitiwa kwa namna ya pekee ili kukomesha matukio hayo. Kauli hiyo imetolewa leo  Julai 26, 2024 jijini Mwanza, katika tamko la pamoja lililotolewa na mashirika  55  yanayojishughulisha na utetezi wa haki za binadamu kutoka mikoa ya kanda ya ziwa Geita, Mwanza, Mara, Simiyu na Shinyanga baada ya kumalizika kwa mafunzo na mkutano mkuu wa Mwaka wa kanda, ulifanyika katika hotel ya Gold Crest kwa kwa uratibu na ufadhiliwa na THRDC. Tamko hilo limesomwa kwa niaba ya wenzake na Edwin Soko, mwanachama wa mtandao huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za kupiga vita dawa za kulevya na uharifu nchini Tanzania....

Dkt. Mwinyi Tusimamie Malezi Yenye Maadili Kwa Vijana

RAIS wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Wazazi na Walezi kuhakikisha wanasimamia malezi bora yenye maadili kwa watoto na  vijana. Alhaj Dk. Mwinyi  aliyasema hayo leo Julai 26 , 2024 alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika ibada ya sala ya Ijumaa  msikiti wa Sheikh Sharaan Meli nne Unguja. Aidha Dk.Mwinyi ameleeza kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anasimamia malezi ya watoto na vijana kutokana  kwa kuwa dunia imebadilika na sasa ni wakati wa utandawazi, hujifunza mengi kupitia mitandao ya kijamii.   Rais Dk.Mwinyi amewataka Wazazi na walezi kuhakikisha  wanawafundisha watoto na vijana  elimu ya Dini ili kuwa taifa lenye raia wema na hofu ya Mungu. Kwa upande mwingine Rais Dk. Mwinyi amehimiza kuendelea kuiombea nchi kudumisha amani,utulivu, umoja na mshikamano ili kuzidi  kupiga hatua ya maendeleo.