Na. Mwandishi wetu,MWANZA Shule ya Santa Edwin Pre and Primary School ya Majengo Mapya, Nyegezi jijini Mwanza, imefanya mahafali yake ya tatu, ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha hatua muhimu ya masomo kwa wanafunzi pamoja na kutambua mchango wa walimu, wazazi na uongozi wa shule. Mahafali hayo yaliyofanyika Septemba 24, 2026, yalihudhuriwa na wageni mbalimbali, huku Barkat Firoz Khan, Afisa Rasilimali Watu kutoka Furaha Company Ltd ya jijini Mwanza, akiwa Mgeni Rasmi. Akizungumza katika hafla hiyo, Khan aliipongeza Santa Edwin kwa juhudi inazofanya katika kuboresha kiwango cha elimu na matokeo ya wanafunzi katika mitihani mbalimbali, ikiwemo mitihani ya kitaifa. Alisema mafanikio ya shule hayawezi kutenganishwa na ushirikiano wa karibu kati ya walimu, wazazi na wanafunzi, akisisitiza umuhimu wa kujenga mazingira yanayochanganya ufaulu wa kitaaluma na malezi yenye maadili. “Nashauri walimu, watoto na wazazi kuendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha shule inatoa watoto wenye ufaulu m...
Marato tv - Sauti ya Jamii