Skip to main content

Posts

Showing posts from June 21, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

RAIS DKT. MWINYI AKUTANA NA JAJI MKUU MASAJU, ASISITIZA MAGEUZI YA KIDIJITALI MAHAKAMANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika utendaji wa Mahakama ni eneo muhimu linalopaswa kupewa kipaumbele ili kuharakisha upatikanaji wa haki na kuongeza ufanisi. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 22 Juni 2026, alipokutana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Jaji George Masaju, aliyefika Ikulu Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha. Amesema Mahakama ya Zanzibar ina fursa ya kujifunza kutokana na mafanikio yaliyofikiwa na Mahakama ya Tanzania katika matumizi ya Tehama, kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati na kupunguza gharama za kiutendaji. Rais Dkt. Mwinyi amepongeza ushirikiano uliopo baina ya Mahakama ya Zanzibar na Mahakama ya Tanzania na kusisitiza umuhimu wa kuuendeleza ili kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya pamoja kwa manufaa ya wananchi. Aidha, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mkazo katika matumizi ya Tehama na uimarish...

RAIS WA NAMIBIA: TUIDUMISHE URITHI WA UKOMBOZI, SASA TUJIKOMBOE KIUCHUMI

 Rais wa Jamhuri ya Namibia, Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, amesema kuwa historia ya Tanzania katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika itaendelea kubaki alama isiyofutika, akisisitiza kuwa baada ya ushindi wa ukombozi wa kisiasa, mataifa ya Afrika yanapaswa kuelekeza nguvu zake katika kujikomboa kiuchumi kupitia mshikamano, ushirikiano na maendeleo ya pamoja. Akizungumza leo Jun 21,2026 wilayani Kongwa Mkoani Dodoma alipotembelea Makaburi na Kambi ya Kihistoria ya wapigania uhuru wa Chama cha SWAPO wilayani Kongwa, mkoani Dodoma, Rais Dkt. Nandi-Ndaitwah amesema Tanzania iliandika historia ya kipekee kwa kuwafungulia milango wapigania uhuru, kuwapatia ardhi ya kuishi na kufanya mafunzo, pamoja na kuwalinda hadi walipofanikisha ukombozi wa Namibia na mataifa mengine ya Kusini mwa Afrika. Amesema wananchi wa Namibia wataendelea kuikumbuka Tanzania kwa mchango wake mkubwa, akibainisha kuwa uhusiano wa nchi hizo mbili haujajengwa kwa misingi ya diplomasia pekee, bali umejengwa kwa h...

WAZIRI MKUU AWASISITIZA WATANZANIA KUWAHUDUMIA WENYE MAHITAJI

 _Asema mambo ya kutegemea wahisani yamepitwa na wakati_   WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania kushirikiana na Serikali katika kutunza na kuhudumia vituo vya watoto wenye mahitaji maalumu na wasiojiweza badala ya kutegemea wahisani kutoka nje kwani mambo hayo yamepitwa na wakati. Ametoa kauli hiyo leo Jumapili, Juni 21, 2026 katika harambee ya uchangiaji wa jengo la kitega uchumi cha kanisa la Anglika jijini Dodoma. “Mambo ya misaada yamepitwa na wakati na hata katika bajeti Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kusisitiza kuwa na bajeti ya nchi ambayo inategemea rasilimali za ndani ya nchi”.  Pia, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametoa rai halmashauri zote nchini ziandae orodha ya vituo vya kulelea watoto wenye mahitaji maalumu na wasiojiweza na kuona namna ya kuvisaidia ambapo amesisitiza si vema kuwaandikia watu hao barua za kwenda kuomba misaada pindi wanapofika kwenye ofisi za umma. Waziri Mkuu amesema awali katika maeneo mbalimbali nchini ili...

UKAGUZI WA LESENI ZA MADINI WAIMARISHA UZINGATIAJI WA SHERIA NCHINI

 📍DODOMA Tume ya Madini imeendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa leseni za madini nchini kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya leseni hizo na kuhakikisha shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini zinafanyika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa. Akizungumza katika Banda la Tume ya Madini kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park mkoani Dodoma, Mtakwimu kutoka Kurugenzi ya Leseni ya Tume ya Madini, Azihar Kashakara, amesema ukaguzi huo ni muhimu katika kuhakikisha wamiliki wa leseni wanatimiza masharti na wajibu unaotokana na leseni walizopewa. Amesema kuwa, pamoja na kufuatilia maendeleo ya leseni, Kurugenzi ya Leseni ina jukumu la kutoa na kusimamia leseni za madini, kutafsiri na kusambaza takwimu za leseni, pamoja na kuwezesha ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo na umiliki wa leseni hizo. Kashakara ameeleza kuwa utoaji wa leseni za madini unazingatia masharti na vigezo vilivyowekwa kisheria, hi...

PANGANI YAPATA 'CLEAN SHEET' MIRADI YA MWENGE 2026

 NA: MWANDISHI WETU, PANGANI Kiongozi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026, Wazo Mwang'onda, ameridhishwa na ubora wa miradi ya maendeleo pamoja na thamani ya fedha (value for money) zilizotumika kutekeleza miradi hiyo katika halmashauri ya wilaya ya Pangani mkoani Tanga. Kiongozi huyo ameyasema hayo Juni 20, 2026, ambapo amesisitiza kuwa miradi yote iliyotekelezwa katika halmashauri hiyo ina ubora, jambo linalothibitisha umakini wa viongozi katika kusimamia miradi ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi na kuchochea maendeleo nchini. "Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026, umeridhishwa na miradi ya maendeleo iliyotekelezwa Pangani. Hongereni sana viongozi kwa usimamizi mzuri," amesema Mwang'onda. Katika hatua nyingine, Mbunge wa Jimbo la Pangani na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema, viongozi ndani ya halmashauri ya Pangani wako makini linapokuja suala lenye maslahi kwa wananchi. "Tunampongeza Rais wetu, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo,...