Musoma. Serikali mkoani Mara imiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuanzisha Mamlaka ya Uhifadhi wa ziwa Victoria hatua ambayo itasaidia uhifadhi na uendelevu wa ziwa hilo ambalo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa mkoa na watu wake. Ombi hilo limetolewa mjii Musoma leo Jumanne Agosti 11 2026 na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Bashiru Ally ambaye yupo mkoani Mara kwa ziara ya siku nne. Kanali Mtambi amesema kutokana na shughuli za kiuchumi na kijamii zinazofanywa ndani ya ziwa hilo ipo haja ya kuwa na mamlaka maalumu itakayokuwa inasimamia ziwa hilo ili shughuli hizo ziweze kufanyika kwa ufanisi na kuleta tija zaidi bila kuathiri uhai wake. Ametolea mfano suala la ufugaji wa vizimba ambalo limepata mapokeo makubwa mkoani Mara baada ya Serikali kuanza kuwezesha wavuvi ambapo amesema vijana wengi hivi sasa wameamua kujiajiri kupitia ufugaji huo ndani ya ziwa hilo hivyo ipo haja ya kuwa na mamlaka rasmi itakayosimamia rasilimali hiyo muhimu. "Kuhus...
Marato tv - Sauti ya Jamii