Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Ndugu Gerald Kusaya, leo tarehe 11,septemba 2026, ameongoza hafla ya kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Brigedia Jenerali Evans Alfred Mtambi, kufuatia kupandishwa cheo chake cha kijeshi kutoka Kanali hadi Brigedia Jenerali. Hafla hiyo imefanyika katika viunga vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali, watumishi wa umma, viongozi wa dini pamoja na wadau wengine wa mkoa. Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Ndugu Gerald Kusaya, ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuupa kipaumbele Mkoa wa Mara na kuwaamini viongozi wenye uwezo na uadilifu. Amesema kupandishwa cheo kwa Mkuu wa Mkoa ni ishara ya kutambua weledi, uhodari, utii na utumishi wake uliotukuka katika kulitumikia taifa. “Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuupa kipaumbele Mkoa wa Mara. Kupandishwa cheo kwa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ni heshima kubw...
Marato tv - Sauti ya Jamii