Skip to main content

Posts

Showing posts from September 29, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

KIRUSWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU QATAR

  *Kiwanda chazalisha hadi kilo 500 za dhahabu kwa siku* *Tanzania, Qatar kujenga ushirikiano katika uwekezaji na uongezaji thamani madini* *Wafanyabiashara wa Tanzania wahamasishwa kutumia fursa za soko la kimataifa* *📍Doha, Qatar* Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, ametembelea Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu cha Falcon Gold and Precious Metals Refinery kilichopo jijini Doha, Qatar, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutathmini fursa za uwekezaji na uongezaji thamani madini kati ya Tanzania na Qatar. Dkt. Kiruswa ametembelea kiwanda hicho akiwa ameambatana na wafanyabiashara wa madini ya vito kutoka Tanzania kwa ajili ya kushiriki na kujifunza mbinu mbalimbali katika Maonesho ya Kimataifa ya Vito na Saa ya Doha (Doha Jewellery & Watches Exhibition – DJWE) 2026, yaliyoanza  Septemba 28 hadi Oktoba 3, 2026. Kiwanda hicho kina uwezo wa kusafisha hadi kilo 500 za dhahabu kwa siku, huku kikipokea malighafi kutoka nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kusafisha na kuongez...

KIRUSWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU QATAR

 *Kiwanda chazalisha hadi kilo 500 za dhahabu kwa siku* *Tanzania, Qatar kujenga ushirikiano katika uwekezaji na uongezaji thamani madini* *Wafanyabiashara wa Tanzania wahamasishwa kutumia fursa za soko la kimataifa* *📍Doha, Qatar* Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, ametembelea Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu cha Falcon Gold and Precious Metals Refinery kilichopo jijini Doha, Qatar, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutathmini fursa za uwekezaji na uongezaji thamani madini kati ya Tanzania na Qatar. Dkt. Kiruswa ametembelea kiwanda hicho akiwa ameambatana na wafanyabiashara wa madini ya vito kutoka Tanzania kwa ajili ya kushiriki na kujifunza mbinu mbalimbali katika Maonesho ya Kimataifa ya Vito na Saa ya Doha (Doha Jewellery & Watches Exhibition – DJWE) 2026, yaliyoanza  Septemba 28 hadi Oktoba 3, 2026. Kiwanda hicho kina uwezo wa kusafisha hadi kilo 500 za dhahabu kwa siku, huku kikipokea malighafi kutoka nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kusafisha na kuongeza...

MWAMPOSA KUSHIRIKI MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA

 Na Wellu Mtaki, Geita MCHUNGAJI Bonifance Josephat Mwamposa, ambaye pia ni mmoja wa wachimbaji wa madini, anatarajiwa kushiriki katika Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, huku wachimbaji na wadau wa sekta hiyo wakihimizwa kujitokeza kwa wingi. Mwamposa anatarajiwa kuwasili katika viwanja vya EPZA, eneo la Viwanja vya Samia Suluhu Hassan, jijini Geita, siku ya Ijumaa, Oktoba 2, 2026, akiwa ameambatana na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Tanzania, John Wambura. Akizungumza kuhusu maandalizi ya siku hiyo, Katibu wa Chama cha Wachimba Madini Mkoa wa Geita, Misana Nyabange, alisema ujio wa viongozi hao utatoa fursa kwa wachimbaji, watoa huduma na wadau wengine wa sekta ya madini kukutana, kubadilishana uzoefu na kujadili namna ya kuongeza ushiriki wa Watanzania katika kunufaika na rasilimali za madini. Nyabange alisema siku hiyo imeandaliwa kwa lengo la kuimarisha ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya madini na kutoa nafasi kwa wadau kujadili f...

NMB YAPANUA FURSA ZA FEDHA KWA WACHIMBAJI WADOGO , YATOA MIKOPO HADI ASILIMIA 100 YA VIFAA VYA UCHIMBAJI.

 Na. Wellu Mtaki,Dodoma Benki ya NMB imeendelea kuweka msisitizo katika kuwawezesha wachimbaji wadogo na wafanyabiashara wanaotoa huduma kwenye migodi kwa kuwapatia mikopo, elimu ya fedha pamoja na ushauri wa kibiashara, hatua inayolenga kuongeza uwezo wao wa kukuza shughuli zao.  Akizungumza kuhusu huduma hizo, Deogratius Shirima kutoka Idara ya Biashara ya NMB Makao Makuu, amesema benki hiyo ina dawati maalum linaloshughulikia biashara na huduma mbalimbali zinazowalenga wateja wanaofanya shughuli katika sekta ya migodi. Shirima amesema NMB imekuwa ikitoa mikopo kwa wachimbaji wadogo kwa masharti na riba nafuu, huku ikiambatanisha huduma hizo na elimu kuhusu mazingira, fedha na masuala ya ardhi. “Kwa wachimbaji wadogo tunatoa mikopo yetu kwa riba nafuu Lakini pia tunatoa elimu ya mazingira, elimu ya fedha na elimu ya ardhi, kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali,” amesema Shirima. Ameongeza kuwa NMB pia inaangalia namna ya kurahisisha upatikanaji wa mitaji kwa waf...

TANESCO YATAKIWA KUONGEZA ELIMU YA NISHATI SAFI KWA WANANCHI

 Na Wellu Mtaki, Geita Jumuiya za mazingira zimeitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuongeza na kuendeleza ushirikiano na wananchi katika kutoa elimu kuhusu matumizi ya nishati safi, huku zikitaka jamii kueleweshwa namna matumizi ya nishati hiyo yanavyoweza kuchangia katika utunzaji wa mazingira na maendeleo ya kiuchumi. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chato mkoani Geita, Peter Lous, alipotembelea banda la TANESCO katika Maonesho ya Tisa ya Madini yanayofanyika mkoani Geita  ambapo TANESCO imewasilisha teknolojia mbalimbali, ikiwemo majiko yanayotumia umeme, yanayolenga kupunguza matumizi ya nishati zinazochangia uharibifu wa mazingira.  Lous amesema ushirikiano kati ya Serikali, taasisi na wananchi ni muhimu katika kuhakikisha mipango ya nishati na mazingira inatekelezwa kwa ufanisi na kuleta matokeo yanayotarajiwa. Amesema wananchi wanahitaji kupewa elimu ya kutosha kuhusu teknolojia hizo ili waweze kuzifahamu, kuzitumia kwa usahihi na kushiriki kikamilifu...

TEKNOLOJIA MPYA YA MILIPUKO YABADILI SEKTA YA UCHIMBAJI , KAMPUNI YAONGEZA HUDUMA KWA WACHIMBAJI

 Na Wellu Mtaki, Geita KAMPUNI inayojihusisha na uuzaji wa vifaa na utoaji wa huduma za kitaalamu katika sekta ya uchimbaji imeanza kutumia teknolojia mpya za milipuko zinazolenga kuwasaidia wachimbaji kukabiliana na changamoto za mazingira na kufikia maeneo ambayo awali yalikuwa magumu kufikika. Teknolojia hiyo, ikiwamo matumizi ya mashine za MMU, imeelezwa kuwa inaweza kutumika katika mazingira yenye kiwango kikubwa cha maji, hivyo kuwapa wachimbaji fursa ya kutumia teknolojia inayolingana na mazingira ya eneo husika. Afisa Masoko wa ESEH INVESTMENTS, William Sisty, amebainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Tisa ya Madini yanayofanyika mkoani Geita, mara baada ya kampuni hiyo kutembelewa na Mkuu wa Wilaya ya Chato. Sisty amesema kampuni hiyo, ambayo imekuwa ikitoa huduma tangu mwaka 2014, imeendelea kuwekeza katika teknolojia na vifaa vya kisasa ili kukidhi mahitaji ya wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa. “Tumekuwa tukijikita katika kuwahudum...