Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi wa Wasafi Media, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz, ameipongeza Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) kwa utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari, huku akiahidi kuwa tayari kufuata matakwa yote ya kisheria yanayohusu sekta ya habari na watumishi wake. Akizungumza baada ya kufika katika ofisi za Bodi hiyo kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria, Diamond amesema Wasafi Media haina nia ya kukwepa utekelezaji wa Sheria, bali iko tayari kushirikiana kikamilifu na wasimamizi wa taaluma hiyo. Amesema licha ya Sheria ya Huduma za Habari kuathiri vyombo vya habari kwa namna moja au nyingine, haiwezi kupingwa kwani ilitoa muda wa kutosha kwa wadau kujipanga na kutimiza vigezo vilivyowekwa ikiwemo Waandishi wake kuwa na kiwango cha Elimu cha Diploma na kuendelea. Diamond amekiri kuwa ujio wa Bodi ya Ithibati umeleta nidhamu kubwa katika taaluma ya habari, akisisitiza kuwa Wasafi Media inaunga mkono...
Marato tv - Sauti ya Jamii