Skip to main content

Posts

Showing posts from August 28, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Miradi Saba ya Maendeleo yenye Thamani ya Billioni 2.5 kupitiwa na Mwenge wa Uhuru

Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 kukimbizwa umbali wa Kilomita 80.3 katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Johari Samizi wakati akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe, Ngwilabuzu Ludigija mapema Leo tarehe 29/8/2025. Mhe.Samizi ameeleza kwamba Mwenge wa Uhuru utakagua, Utazindua na kuweka Jiwe la msingi katika Miradi 7 ya Sekta mbalimbali zikiwemo Afya,Elimu, Miundombinu, Nishati, Mazingira, Maji na Vijana yenye gharama ya zaidi ya Shilingi Bilioni 2.5. Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 Ndugu Ismail Ali  Ussi ameridhishwa na utayari na Mapokezi  ya Wananchi wa Wilaya ya Misungwi pamoja na juhudi zinazofanywa na Watendaji katika utekelezaji wa Miradi mbalimbali na kuwahimiza Wananchi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu Mwezi oktoba mwaka huu na kutimiza haki ya kikatiba ya kupiga kura kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge na Madiwani. Kauli mbiu ya Mbio z...

Dkt. Nchimbi Atia Mguu Mwanza Kuomba Kura Kuelekea Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu,Mwanza  Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi  amewasili Mkoa wa Mwanza Leo Agosti 29, 2025 kwa ajili ya Kampeni kuelekea Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.  Balozi Dkt Nchimbi anatarajia kufanya mikutano mbalimbali kwa ajili ya kuzinadi sera pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ya 2025-2030. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeingia siku ya pili za kampeni zake baada ya jana kuzinduliwa rasmi hapo jana jijini Dar es Salaam  na Mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan 

Matibabu ya Kisukari, Moyo, Saratani, Figo Yatakuwa Bure

Katika siku zake Mia moja za mwanzo madarakani Ikiwa Wananchi wa Tanzania watampatia ridhaa ya kuongoza tena serikali, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan, amebainisha kuwa atafanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya nchini, ikiwa ni pamoja na  kugharamia kwa asilimia mia moja vipimo na matibabu ya kibingwa kwa wagonjwa wa saratani, figo, moyo, Sukari, mifupa na mishipa ya fahamu. Aidha katika kutekeleza sheria ya bima ya afya kwa wote, ndani ya Siku mia moja za mwanzo ikiwa atashinda uchaguzi Mkuu, Rais Samia pia ameahidi kuzindua rasmi mfumo wa taifa wa bima ya afya kwa wote kwa awamu ya majaribio kwa kuanza na wazee, watoto, wajawazito pamoja na watu wenye ulemavu, akisema gharama za matibabu kwa makundi hayo ya jamii zitabebwa na mfuko wa Taifa wa bima ya afya kwa wote. Wakati akiainisha vipaumbele vyake ndani ya siku mia moja ikiwa ataibuka mshindi katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Rais Samia kwenye ...

Wanafunzi 100 Global Education Link wapaaa majuu kuanza masomo

Na Mwandishi Wetu WANAFUNZI 100 wamesafiri kwenda kwenye vyuo vikuu mbalimbali nchini India kwa mwaka huu wa masomo kupitia Global Education Link. Meneja Mkuu wa GEL, Regina Lema alisema taasisi hiyo imekuwa na kawaida ya kuwasindikiza wanafunzi hao hadi kwenye vyuo wanavyokwenda na kuhakikisha wanapata malazi. Alisema lengo ni kuhakikisha wanafunzi wamefika salama na kupata usili chuoni kwani ni humuma ambazo taasisi ya GEL imekuwa ikitoa kwa wanafunzi hao. Alisema tarehe 10 mwezi wa tisa kundi lingine la wanafunzi 100 litaondoka kwenda nchi za China na Malasyia na watasindikizwa na watumishi wa Global “Huu ni mwanzo wa wanafunzi kuondoka kwasababu kila  baada ya siku 10 wanafunzi watakuwa wanaondoka kwenda nnje ya nchi kwa hiyo mwanafunzi ambaye hujapata udahili kusoma nje ya nchi uje GEL kupata nafasi kwenye vyuo nje ya nchi,” alisema Regina alisema wamekuwa wakiwapa wanafunzi mikopo isiyo na riba ili kuwapunguzia msongo wa mawazo pale wanapokuwa na changamoto ya kulipa ada. “Mk...

Khalid Nsekela Ateuliwa Kugombea Ubungr Jimbo la Kyerwa

  Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Kyerwa mkoani Kagera,Mwalimu Ramadhan Marwa amemteua mgombea wa chama cha Mapinduzi (CCM) Khalid Mussa Nsekela kugombea ubunge katika jimbo hilo. Mwalimu Marwa ametangaza uteuzi huo mara baada ya kukamilika kwa mchakato wa uchambuzi na uhakiki wa wagombea walioonesha nia ya kuwania nafasi hiyo. Marwa amesema Nsekela ametimiza vigezo vyote vinavyotakiwa kikatiba,  kisheria,kikanuni na kuwasilishaji nyaraka sahihi. Nsekela mwenye shahada ya uzamili katika usimamizi wa biashara na masoko ya kimataifa na shahada ya uzamili ya dipromasi ya uchumi katika mahojiano mafupi baada ya uteuzi huo, ameahidi kufanya kampeni za kistaarabu,kudumisha amani,upendo na kuzingatia hoja na masuala ya msingi yatakayomuongoza kutatua changamoto zinazowakabili  wakazi wa Kyerwa. Pia ametoa shukrani kwa CCM kuanzia ngazi ya kata hadi Taifa na wananchi wote wa Kyerwa bila kujali itikadi zao za vyama kwa ushirikiano ambao wanaendelea kumpatia na imani ambayo wamem...

Rea yatekeleza kwa vitendo mkakati wa Nishati safi ya kupikia

📌REA KUANZA UUZAJI NA USAMBAZAJI MAJIKO BANIFU 6,488 MKOANI SONGWE 📌MAJIKO BANIFU 1,622 KUSAMBAZWA KILA WILAYA 📍 SONGWE Wakazi wa mkoa wa Songwe waaswa kuunga mkono jitihada za Serikali katika utunzaji wa mazingira na afya zao kwa kutumia nishati safi na salama ya kupikia. Hayo yamebainishwa leo Agosti 28, 2025 wakati wa utambulishaji wa mradi wa usimamizi na usimamizi wa majiko banifu mkoa wa Songwe na mhandisi wa miradi kutoka kwa miradi ya vijijini, Kelvin Tarimo. Mhandisi Tarimo amesema, serikali kupitia wakala wa vijijini imeandaa mpango wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi ya kujifunza ili lengo la zaidi ya asilimia themanini 80% ya watanzania ifikapo 2034 wawe wanatumia nishati safi ya kupikia. Mhandisi Tarimo ameendelea kwa kusema, katika kutekeleza mradi huu, Wakala wa Nishati Vijijini umeandaa mpango wa uuzwaji wa majiko banifu 200,000 kwa bei ya ruzuku yenye ufanisi mkubwa katika utumiaji wake. Kwa mkoa wa Songwe, mradi huu unatarajia kugharimu zaidi ya TZS M...