Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imepitisha rasmi Muongozo kwa wanahabari wakongwe nchini waliokidhi vigezo vya kupatiwa Ithibati ya Maisha kwa lengo la kutambua mchango wao katika sekta hiyo. Mwongozo huo umepitishwa na kuzinduliwa tarehe 11 Julai, 2026 kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, ulioambatana na hafla ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari ( JAB ). Hatua hiyo inakuja kama jawabu la Kilio cha wadau wa habari, kutaka kuwe na namna bora ya kuwatambua wenzao wakongwe kwenye tasnia hiyo ambao walilazimika kukaa kando kazini kwa kutokidhi vigezo vya JAB. Hatua hiyo iliifanya JAB ifanye tathmini na hatimaye imetoa mwongozo ukiwa na masharti mbalimbali yaliyopokewa vyema na waandishi wa habari.
Marato tv - Sauti ya Jamii