Skip to main content

Posts

Showing posts from March 6, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia Aongoza Kikao Cha Baraza la Mawaziri

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Machi, 2025.    

Waziri Mkuu Ampongeza Rais Samia Kwa Mageuzi Makubwa Katika Sekta ya Elimu Nchini

-Aongoza matembezi ya hisani na uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya TET -Ausisitiza uongozi kuongeza wigo wa kuimarisha upatikanaji wa vitabu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza matembelezi ya hisani na uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TET) ambapo amesisitiza uongozi wa taasisi hiyo kuongeza wigo wa kuimarisha upatikanaji wa vitabu kwenye shule zote nchini. Waziri Mkuu amesema anafahamu kuwa TET imedhamiria kuchapa vitabu kwa wingi ili kufikia uwiano wa kitabu kimoja kwa mwanafunzi mmoja, jambo ambalo litaleta  manufaa makubwa katika elimu na Taifa kwa ujumla. “Hivyo, kwa dhamira ya dhati kabisa, sote hatuna budi kuliunga mkono jambo hili.” Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 7, 2025) alipozungumza baada ya kumalizika kwa matembezi ya hisani katika ofisi ya TET, Mikocheni jijini Dar es Salaam, ambapo ametumia fursa hiyo kumpongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mageuzi makubwa aliyoyafanya katika sekta ya elimu nchini.  Mheshi...

Waziri Mkuu Ashiriki Matembezi ya Hisani Ya Miaka 50 ya Tet

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Machi 07, 2025 ameshiriki katika matembezi ya hisani ya kuadhimisha miaka 50 ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), jijini Dar es Salaam Viongozi wengine walioshiriki matembezi hayo ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, Naibu Waziri wa Wizara hiyo Omari Kipanga na watendaji wengine wa Wizara ya Elimu pamoja nawa Taasisi ya Elimu Tanzania. Matembezi hayo yalianzia katika viwanja vya Taasisi ya Elimu na kuishia katika hiyo.  #KitabuKimoja #MwanafunziMmoja

Meet a PhD holder who decided to study at KMTC

Most people see a PhD as the peak of academic achievement. But for 42-year-old Martin Ogwang, it was just another step in his lifelong pursuit of knowledge.   Despite holding a doctorate in Biochemistry, a Master’s in Bioinformatics from Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT), and a Bachelor’s degree from Makerere University, he made an unexpected choice by enrolling at the Kenya Medical Training College (KMTC).   Why would a university don decide to wear a uniform and go back to school?   The Journey Three years ago, on a chilly Tuesday morning, Martin embarked on a journey that would bring him closer to earning a Diploma in Clinical Medicine at KMTC Bungoma Campus.   "I had long desired to join KMTC to study the course, but fate had it otherwise," he says.   "When an opportunity finally presented itself, I grabbed it with open arms. I wore my uniform and set off for College," he continues.   At JKUAT, ...

Rais Samia Ashiriki Mkutano wa Ulinzi na Usalama wa Sadc Kwa Njia ya Mtandao

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ akishiriki Mkutano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya hiyi (SADC Organ) kwa njia ya mtandao, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Machi, 2025. Mkutano huo umejadili masuala ya hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Korea Kusini Yaunga Mkono Matumizi Nishati Safi ya Kupikia

📌 *Rais Samia apongezwa kuwa Kinara wa Nishati Safi* 📌 *Dkt. Biteko asisitiza ushirikiano wa Serikali, Sekta Binafsi* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Mkakati wa Nishati Safi ya kupikia chini ya uasisi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan umeendelea kupigiwa chapuo ambapo Korea Kusini imesema iko tayari kuunga mkono jitihada hizo. Hayo yamebainika leo Machi 6, 2025 katika mazungumzo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Mhe. Ahn Eunju kando ya Mkutano wa Mafuta na Gesi kwa nchi za Afrika Mashariki unaoendelea jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Tanzania imepiga hatua katika kuwezesha wananchi kupata unafuu wa maisha kwa kupata na kutumia nishati safi na hivyo kuepukana na madhara yanayotokana na matumizi ya nishati isiyokuwa safi yakiwemo magonjwa na vifo. Mkakati wa Taifa wa Nishati safi ya kupikia wa mi...

Serikali Inatambua Umuhimu wa Kukuza Usawa wa Kijinsia – Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inatambua umuhimu wa kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kama njia mojawapo ya kuimarisha ustawi na kufikia maendeleo jumuishi na endelevu.  Mheshimiwa Majaliwa amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha jamii ya Watanzania inaishi kwa umoja na mshikamano kati ya wanaume na wanawake na kuwa wote wanapata huduma za msingi kwa haki na usawa katika nyanja zote ikiwemo kisheria, elimu, afya, uchumi na nafasi za maamuzi. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Machi 6, 2025) alipozungumza na wananchi katika Kongamano la wanawake Kanda ya Kusini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika Kitaifa Machi 8, jijini Arusha. Kongamano hilo limefanyika katika viwanja vya Maegesho, Nachingwea mkoani Lindi. Mheshimiwa Majaliwa amesema ili kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi Serikali imeendelea kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri na kutoa mikopo k...

Arusha Wavutiwa na Bidhaa za Nishati Safi ya Kupikia

Wananchi Jijini Arusha wamevutiwa na bidhaa mbalimbali za Nishati Safi ya Kupikia na wameipongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kufikisha bidhaa hizo katika Maonesho yanayoendelea mkoani humo kuelekea Siku ya Wanawake Duniani. Wakizungumza kwa nyakati tofauti Machi 6, 2025 mara baada ya kutembelea Banda la REA na kushuhudia teknolojia mbalimbali za majiko ya Nishati Safi ya Kupikia; wananchi hao wamepongeza uwepo wa teknolojia hiyo ambayo wamesema licha ya kulinda mazingira lakini pia inarahisisha suala zima la kupika na hivyo kurahisisha maisha. "Tumefurahi kuona majiko yaliyoboreshwa, teknolojia iliyotumika ni nzuri, majiko haya tumeyapenda," amesema Ester Mwasigo mkazi wa Dodoma ambaye yupo Jijini humo kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Kimataifa 2025. Mwasigo alitoa wito kwa wananchi kutembea banda la REA ili kujifunza na kuchangamkia bidhaa hizo za Nishati Safi  ikiwa ni hatua moja wapo ya kuunga mkono jitihada na dhamira ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya k...

Serikali inatambua umuhimu wa kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake-Majaliwa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kanda ya Kusini, yanayofanyika katika viwanja vya Maegesho, Nachingwea mkoani Lindi. Akizungumza katika kongamano hilo, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kama njia mojawapo ya kuimarisha ustawi na kufikia maendeleo jumuishi na endelevu.