Skip to main content

Posts

Showing posts from June 1, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WASTAAFU WAVUNA MATUNDA YA MAGEUZI: PENSHENI YA CHINI YAPAA HADI SH. 250,000

 Hatua za Serikali za kuendelea kuboresha maisha ya wastaafu nchini zimezaa matunda baada ya kima cha chini cha pensheni kuongezwa kutoka Shilingi 100,125.87 hadi Shilingi 250,000 kwa mwezi, ongezeko kubwa linalolenga kuongeza ustawi na kuimarisha maisha ya wanufaika wa pensheni wanaolipwa na Hazina. Akiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma leo Juni 2, 2026, mapitio ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya mwaka 2025/26 pamoja na mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2026/27, Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb.), amessema Serikali imeendelea kutekeleza kwa vitendo dhamira yake ya kuhakikisha wastaafu wanapata haki na stahiki zao kwa wakati. Amesema hadi Aprili 2026, Serikali imelipa mafao ya wastaafu yenye thamani ya Shilingi bilioni 577.41, hatua inayodhihirisha uwajibikaji na utayari wa Serikali wa kuheshimu mchango wa watumishi waliolitumikia Taifa kwa miaka mingi. Kwa upande wa hifadhi ya jamii, Serikali pia ililipa michango ya kisheria yenye thama...

TUNALINDA UCHUMI WA TAIFA KWA KUKABILIANA KIKAMILIFU NA FEDHA HARAMU-WAZIRI KHAMIS OMAR

 SERIKALI imeendelea kuimarisha vita dhidi ya utakasishaji wa fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na ufadhili wa silaha za maangamizi kwa kutekeleza mageuzi mbalimbali yanayolenga kuimarisha usalama wa mfumo wa fedha nchini na kulinda uchumi wa Taifa. Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb),wakati akiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma leo Juni 2, 2026, mapitio ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya mwaka 2025/26 pamoja na mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2026/27. "Tumeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha mifumo ya udhibiti wa fedha haramu ili kuhakikisha sekta ya fedha nchini inakuwa salama, yenye uwazi na inayoendana na viwango vya kimataifa," alisema Waziri Omar. Amesema hadi Aprili 2026, Wizara kupitia Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu imefanya mapitio na kuhuisha Tathmini ya Taifa ya Vihatarishi ili kuendana na mabadiliko ya mazingira ya kifedha na kukidhi matakwa ya Kikosi Kazi cha Kimataifa cha Kudhibiti Uta...

RAIS SAMIA AELEKEA NCHINI URUSI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Matukio tofauti ya Picha alipoondoka Katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dar es salaam kuelekea Nchini Urusi kwenye Ziara ya Kitaifa ikiwa ni Mwaliko wa Rais wa Shirikisho la Urusi Mhe. Vladimir Putin Leo Juni 02,2026.

RIDHIWANI AWATAKA MAAFISA TAWALA KUZINGATIA KANUNI NA MIONGOZO YA UTUMISHI

 Na Mwandishi Wetu, Dodoma WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amewataka Maafisa Tawala na Rasilimali Watu nchini kuzingatia kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma ili kuimarisha ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Waziri Kikwete alitoa wito huo jana wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Tawala na Rasilimali Watu uliofanyika katika Ukumbi wa Jenerali Mabeyo jijini Dodoma. Mkutano huo umewakutanisha Maafisa Tawala na Rasilimali Watu kutoka wizara, idara, taasisi za serikali zinazojitegemea pamoja na mamlaka za serikali za mitaa kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali za taaluma yao na kuweka mikakati ya namna bora ya kukabiliana nazo. Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Kikwete alisisitiza umuhimu wa kuimarisha mawasiliano kati ya ofisi za washiriki na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kurahisisha utatuzi wa changamoto zinazojitokeza katika maeneo yao ...

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AWASILI UFARANSA KUONGOZA VIKAO VYA BODI YA GPE

 Paris, Ufaransa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewasili leo nchini Ufaransa kwa ziara ya kikazi ya kushiriki na kuongoza vikao vya Bodi ya Global Partnership for Education (GPE), taasisi ya kimataifa inayojihusisha na maendeleo ya elimu duniani, ambako anahudumu kama Mwenyekiti wa Bodi. Mhe. Kikwete alipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Saidi Othman Yakubu, pamoja na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo. Katika nafasi yake kama Mwenyekiti wa Bodi ya GPE, Mhe. Kikwete anaongoza juhudi za kimataifa zinazolenga kuimarisha upatikanaji wa elimu bora, jumuishi na yenye usawa kwa watoto katika nchi zinazoendelea. GPE ni ushirikiano wa kimataifa unaozileta pamoja serikali, mashirika ya maendeleo, sekta binafsi, asasi za kiraia na wadau wengine wa elimu ili kusaidia nchi zenye kipato cha chini na cha kati kuboresha mifumo yao ya elimu. Kupitia us...

MWAHUTA YAGAWA NYAMA KWA WENYE UHITAJI, YACHINJA NG’OMBE 700 MWAKA HUU

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mkono wa huruma Tanzania (MWAHUTA), Araphaty Japhary Mayala amesema taasisi hiyo imefanikiwa kuchinja takribani ng’ombe 700 mwaka huu kwa ajili ya kugawa nyama kwa makundi mbalimbali yenye uhitaji, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza huduma za kijamii na kusaidia wananchi wasiojiweza. Matendo hayo ya huruma ni kutokana na mafundisho ya dini ya kiislamu kama anavyosema Mwenyezi Mungu katika QUR'AN tukufu inapofika sikukuu ya Eid ul-Adha ni vema kuchinja Mnyama ili Kutoa sadaka Kwa jamii inayokuzunguk Akizungumza jijini Dodoma, wakati akitekeleza ibada ya kuchinja Mayala amessema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau, viongozi wa serikali, viongozi wa mitaa na wananchi walioshiriki kufanikisha zoezi hilo muhimu. Mayala pia Ametoa shukrani za dhati kwa viongozi wote waliowaunga mkono, hususan Mkuu wa Wilaya ambaye alisema amekuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa ulinzi na huduma za madaktari kwa ajili ya...

WANAFUNZI 246,197 WALIOPANGIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO WANAPASWA KURIPOTI SHULENI JULAI 04, 2026 - PROF. SHEMDOE

Na OWM - TAMISEMI, Dar es Salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amesema jumla ya wanafunzi 246,197 wakiwemo wasichana 114,102 na wavulana 132,095 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2026 wanatakiwa kuripoti shuleni kuanzia Julai 04, 2026 hadi Julai 31, 2026 kwakuwa muhula wa kwanza wa masomo utaanza Julai 06, 2026.  Prof. Shemdoe amesema hayo leo Juni 01, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi Ndogo ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Magogoni Jijini Dar es Salaam, wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi kwa mwaka 2026. “Wanafunzi 172,114 sawa na asilimia 69.9 wakiwemo wasichana 85,987 na wavulana 86,127 wenye sifa wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule  za sekondari za Serikali 856 zikiwemo shule za bweni 825, kutwa 25 na kutwa na bweni sita (06),” amefafanua Prof. Shemdoe. Aidha, Prof. S...

RAIS SAMIA ATOA NDEGE YA KUWACHUKUA MASHUJAA SERENGETI BOYS WALIOFIKA FAINALI YA AFCON U-17

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa usafiri wa ndege kwa ajili ya kuwachukua mashujaa wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa Miaka 17 (Serengeti Boys), baada ya kufuzu kucheza fainali ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana (AFCON U-17, 2026) Ndege hiyo itaondoka leo, tarehe 01 Juni 2026, majira ya saa 5:00 usiku, kuelekea nchini Morocco, na itarejea Jumatano tarehe 03 Juni 2026. Msafara huo utaongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda (Mb.) akiwa ameambatana na viongozi wa Serikali pamoja na Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars), lengo ikiwa ni kuongeza nguvu, morali na hamasa kwa Serengeti Boys katika hatua hiyo muhimu. Waziri Mhe. Makonda amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kuendelea kuwekeza katika maendeleo ya michezo nchini pamoja na uamuzi huo wa kurahisisha safari ambayo itaongeza hamasa kwa vijana na kuimarisha uzalendo. Pia amewasisitiza Watanzania kuendelea kuiunga mkono, ...

DKT. MWIGULU ASHIRIKI IBADA YA MAZISHI YA DIWANI AGNES NASANIA WILAYANI IRAMBA

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumatatu Juni 1, 2026 ameshiriki ibada ya mazishi ya Diwani wa Kata ya Shelui, Mhe. Agnes Nasania, iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Shelui, wilayani Iramba mkoani Singida. Akizungumza katika ibada hiyo, Dkt. Mwigulu amesema marehemu Agnes Nasania alikuwa kiongozi jasiri, mkweli na mwenye msimamo katika kusimamia maslahi ya wananchi wa Kata ya Shelui. “Agnes alikuwa kiongozi aliyekuwa tayari kusimamia jambo aliloamini ni sahihi kwa manufaa ya wananchi. Alikuwa na ujasiri wa kusema ukweli na kusimamia maendeleo ya watu wake bila kuyumbishwa,” amesema Dkt. Mwigulu. Amesema mchango wa marehemu katika maendeleo ya Kata ya Shelui utaendelea kukumbukwa na wananchi pamoja na viongozi aliowahi kufanya nao kazi. Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu ameahidi kuendelea kuwa karibu na familia ya marehemu na kusaidia ustawi wa watoto wake ili kuhakikisha wanaendelea na masomo na kutimiza ndoto zao. Aidha, amewataka w...