KIONGOZI MWENGE WA UHURU AIPONGEZA ALLIANCE ONE KWA KUPANDA MITI KWA GHARAMA YA SH.BILIONI 1.2 WILAYANI BUHIGWE
Na Mwandishi Wetu,Kigoma Kampuni ya tumbaku ya Alliance One Tanzania Tobacco Limited imepongezwa kwa kutoa mchango mkubwa katika kuhifadhi mazingira mkoani Kigoma kupitia katika miradi ya kurejesha uoto wa miti katika maeneo yaliyoathiriwa na shughuli za binadamu na mabadiliko ya tabia nchi. Pongezi hizo zimetolewa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2026 Bw.Wazo Mwang’onda, baada ya kukagua mradi wa shamba la miti katika shule ya sekondari Munagana linalofadhiliwa na kampuni hiyo kwa kupanda miti ekari 414 ambapo mpaka sasa gharama za uendeshaji kwenye shamba hilo ni Shilingi 1,264,723,200. Bw. Mwang’onda amebainisha kuwa kitendo cha kampuni ya Alliance One kuamua kuwekeza katika upandaji wa miti ni cha kizalendo na chenye nia ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhifadhi mazingira na kukuza Uchumi wa wananchi kupitia kilimo cha tumbaku na miti. Mwang’onda ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa Alliance One kuendelea kutoa usaidizi wa ujuzi kwa halmshauri za wi...