Na Mwandishi Wetu, Geita GEITA Gold Mining Limited (GGML) imetenga takribani Sh bilioni 1.2 kwa kipindi cha miaka mitatu kusaidia matibabu ya watoto 300 wenye magonjwa ya moyo nchini, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza upatikanaji wa huduma za kibingwa kwa watoto ambao familia zao zinaweza kushindwa kumudu gharama za matibabu. Kupitia makubaliano yaliyosainiwa leo katika ofisi za makao makuu ya Geita Gold Mining Limited (GGML) mkoani Geita, kati ya GGML na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), kampuni hiyo itatoa takribani Sh milioni 400 kila mwaka kusaidia matibabu ya watoto 100 wenye matatizo ya moyo, hivyo kufikisha jumla ya takribani watoto 300 ndani ya kipindi cha miaka mitatu. Ushirikiano huo umefikiwa kwa uratibu wa Global Medicare ya jijini Dar es Salaam, ambayo imekuwa ikiunganisha wadau na kuhamasisha upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya kusaidia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo nchini. Makubaliano hayo yanaongeza nguvu katika juhudi za Serikali na wadau w...
Marato tv - Sauti ya Jamii