CHATANDA: MAMA TIBAIJUKA, TUJENGE MSINGI WA UTII WA SHERIA NA SI MASHINIKIZO YA KUFUTA KESI KWA JINA LA MARIDHIANO
NA: MWANDISHI WETU Mwenyekiti Taifa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda, amemshauri aliyewahi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, kuwa balozi wa kuhimiza viongozi na wananchi kutii sheria za nchi ili kuepuka kuingia katika mikono ya vyombo vya sheria. Chatanda ameyasema hayo Julai 14, 2026, kufuatia ujumbe alioandika Prof. Tibaijuka katika Mtandao X, kuhusiana na kesi inayomkabili Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu. Katika ujumbe wake, Prof. Tibaijuka amesema "Dkt. Samia Suluhu, Mhe. Rais naendelea kushauri kwa dhati Tundu Lissu aachiwe huru kwani kesi haikamiliki, hekima na busara iliyotufanya kuitangaza sera ya 4Rs ulipoingia madarakani ikuongoze tena katika jambo hili". "Simulizi hizi za kutisha za vyombo vya habari vya kimataifa zinainua hisia kali hasa kwa vijana, hata wazee tumekumbushwa kadhia ya operation Sogeza na iliyounda Vijiji vya Ujamaa 1974-1976, taarifa hizi z...