Skip to main content

Posts

Showing posts from June 16, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WAHANDISI TANROADS, TARURA WATAKIWA KUTUMIA MIFUMO MIPYA KULINDA BARABARA

 📍Ampongeza Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha barabara nchini Na Mwandishi Wetu, Mbeya  SERIKALI imewagiza mameneja na wahandisi wa TANROADS na TARURA nchini kutumia mifumo mipya ya kielektroniki kulinda hifadhi za barabara na kutekeleza miradi kwa viwango. Agizo hilo limetolewa Jijini Mbeya Leo Juni 17 2026  na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Solomon Itunda, wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Beno Malisa, kufungua mafunzo ya viongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA). Mafunzo hayo ya siku nne yaliyoanza Jumatatu, Juni 15, 2026, yamewakutanisha Mameneja, Wahasibu, na Wahandisi kutoka mikoa ya kimkakati ya kiuchumi ikiwemo Mbeya, Songwe, Rukwa, Ruvuma, Mtwara, na Lindi. Teknolojia na Udhibiti wa Miundombinu Mhe. Itunda amebainisha kuwa lengo kuu la semina hiyo ni kuwajengea uwezo viongozi hao katika kusimamia miradi ya miundombinu kwa ufanisi, hasa kupitia matumizi ya mfumo mpya wa kielektroniki unaod...

ZUNGU AWATAKA WABUNGE WANAWAKE KUONGOZA MAPINDUZI YA NISHATI SAFI

   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, ameuagiza Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWG) kutumia ushawishi wao katika jamii kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kulinda afya za wananchi, kuhifadhi mazingira na kuharakisha utekelezaji wa ajenda ya taifa ya nishati safi. Akifungua mafunzo ya wabunge hao yaliyoandaliwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) leo Jun 16,2026 jijini Dodoma, Spika Zungu amesema bado kuna dhana potofu zinazowazuia wananchi wengi kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi, hivyo akawataka wabunge kuwa mabalozi wa mabadiliko hayo katika maeneo yao. Amesema baadhi ya wananchi wanaamini kimakosa kuwa nishati safi ni ghali, ngumu kutumia na huathiri ladha ya chakula, jambo ambalo si la kweli.  Sambamba na hayo amewataka wabunge hao kwenda kwa wananchi na kutoa elimu sahihi ili kuondoa mitazamo hiyo na kusaidia kufikia lengo la Serikali la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya ku...

JESHI LA MAGEREZA LASHIRIKI MAADHIMISHO YA KITAIFA YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026

 Na. Ssgt Mawazo Mtondo - Dodoma. Jeshi la Magereza kwa mara nyingine tena linashiriki kikamilifu kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2026 Maadhimisho ambayo ni moja ya Maazimio ya Umoja wa Afrika (AU).  Hivyo, Jeshi la Magereza linawakaribisha wananchi wote wa Tanzania kutembelea Banda la Magereza katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma kuanzia Leo Juni 16 hadi 23, 2026. Maonesho hayo yatawakutanisha Wananchi, Taasisi za Umma na Wadau mbalimbali kwa lengo la kuelezea Dhima, Dira, Mafanikio, Changamoto zilizopo katika suala zima la urekebishaji Wafungwa, kutoa  huduma na taarifa mbalimbali muhimu kuhusu shughuli zinazotolewa na Serikali kwa Wananchi  kupitia Jeshi la Magereza na kuueleza Umma juu ya Mageuzi ya kisayansi yanayofanywa sasa na Jeshi katika uendeshaji na urekebishaji Wafungwa. Pamoja na kutoa huduma hizo, Jeshi la Magereza kupitia Maadhim...

MWAKIOJA ATIKISA BUNGENI, AANIKA SIRI YA IDRAS NA ETS KUKUSANYA TRILIONI 6

 📍Aishauri Serikali kutouogopa mfumo wa Idras ili nchi ijitegemee kwa bajeti kwa asilimia 100 bila mikopo Na Mwandishi Wetu, Dodoma MBUNGE wa Mkinga, Mheshimiwa Twaha Said Mwakioja, ameitaka Serikali kubadilisha mifumo ya kodi na kupeleka mabilioni ya kilimo moja kwa moja kwa wananchi vijijini. Ametoa mchango huo mzito wa kiuchumi leo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya Serikali, huku akijikita katika maeneo makuu mawili ya dharura: Dira ya Taifa ya Maendeleo na Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani. Dira ya 2050 na Mageuzi ya Kilimo Mheshimiwa Mwakioja alibainisha kitalamu kuwa Dira ya 2025 inayoelekea ukingoni ilikuwa nzuri kiuandishi, lakini imeshindwa kufikia lengo la kuondoa umasikini wa chakula kwa asilimia 0, kwani takwimu za sasa zinaonyesha umasikini huo bado umeganda asilimia 8. Ameishauri Serikali kuelekea Dira mpya ya 2050, nchi inahitaji uchumi jumuishi na shirikishi utakaofuta umasikini vijijini kwa asilimia 100, huku nguzo kuu ikiwa ni Kilimo, Ufugaji, na Uvu...

SERIKALI YASISITIZA ULINZI NA HAKI ZA WATOTO

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema kuwa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ni ukumbusho muhimu kwa jamii kuhusu wajibu wa kulinda, kuendeleza na kuhakikisha haki za watoto zinazingatiwa ipasavyo, sambamba na kuenzi mapambano ya watoto wa Soweto waliopigania haki ya kupata elimu bora nchini Afrika Kusini. Akizungumza Juni 16, 2026 jijini Dodoma, Prof. Mkenda ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuweka elimu kama kipaumbele kikuu, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 pamoja na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anayesisitiza kuwa kila mtoto wa Kitanzania anapaswa kupata elimu bila ubaguzi. Amesema Serikali imeimarisha jitihada za kuhakikisha usawa na ujumuishi katika sekta ya elimu, hususan kwa watoto wote wakiwemo wasichana, ili kuwawezesha kupata fursa sawa ya kujifunza na kufikia malengo yao ya maisha. “Hakuna mtoto atakayeachwa nyuma katika mfumo wa e...

NSSF IMEWAOMBA WABUNGE KUPANUA WIGO WA HIFADHI YA JAMII

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, amewaomba Waheshimiwa Wabunge kutumia majukwaa yao kuhamasisha wananchi, hususani waliojiajiri, kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ili waweze kunufaika na huduma na mafao mbalimbali yanayotolewa na mifuko hiyo. Amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza wigo wa hifadhi ya jamii kwa makundi ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakishiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa, lakini bado hayajafikiwa ipasavyo na huduma za hifadhi ya jamii. Bw. Mshomba ameeleza kuwa kuongezeka kwa wanachama katika mifuko ya hifadhi ya jamii kutasaidia juhudi za Serikali za kupunguza umaskini wa kipato, kuongeza tija katika uzalishaji mali, kukuza uchumi wa nchi na kuimarisha ustawi wa wananchi. Kauli hiyo ameitoa leo Juni 15, 2026, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, wakati wa mafunzo maalumu kwa Waheshimiwa Wabunge yaliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana...

WAKAGUZI WA CAF WARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MABORESHO YA VIWANJA VYA AFCON 2027

 Wakaguzi kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Bw. Lakshmikanth Karunanithi na Bw. Eduard Captan, wamefanya ukaguzi wa miundombinu ya viwanja vinavyotarajiwa kutumika katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), na kueleza kuridhishwa na hatua ya maboresho yanayoendelea. Katika ziara hiyo, wakaguzi hao walitembelea Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo walikagua maendeleo ya maboresho ya sehemu ya kuchezea (pitch), maeneo maalumu ya wageni na viongozi mashuhuri (VVIP), pamoja na sehemu zitakazotumika na wanahabari wakati wa mashindano. Mbali na Uwanja wa Benjamin Mkapa, ujumbe huo pia ulitembelea viwanja vya mazoezi vya Gymkhana II na Faras, ambavyo vinajiandaliwa kuhudumia timu zitakazoshiriki AFCON 2027. Baada ya ukaguzi huo, wakaguzi wa CAF walieleza kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa maboresho pamoja na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu hiyo, wakibainisha kuwa hatua zilizofikiwa zinaonyesha dhamira ya kuhakikisha viwanja vinakidhi viwango vinavyohitajika ...

TANZANIA NA CANADA KUSHIRIKIANA KWENYE UTAFITI WA KINA WA MADINI NCHINI

 ▪️Serikali ya Canada yavutiwa na MINING VISION 2030 ▪️Utafiti kugusa mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kaskazini ya Tanzania ▪️Waziri Mavunde awaelekeza GST kuainisha maeneo ya kimkakati ▪️Tafiti za kina za madini kuondoa uchimbaji wa kubahatisha ▪️Tanzania yajipanga kufikisha eneo la utafiti kutoka 16% kwenda 50% ifikapo 2030 *📍Dodoma* Tanzania na Canada zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya utafiti wa kina wa madini, hatua inayotarajiwa kuongeza upatikanaji wa taarifa sahihi za kijiolojia, kuhamasisha uwekezaji na kuendeleza Sekta ya Madini nchini. Hayo yameelezwa leo Juni 16, 2026 jijini Dodoma na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, wakati wa kikao chake na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Emily Burns, kilicholenga kujadili namna ya kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika eneo la utafiti wa madini. Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Mavunde amesema Tanzania hivi sasa inajipanga kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha...

JAB: TEKNOLOJIA ISITUMIKE KUHARIBU UBORA WA HABARI

 Na Mwandishi Wetu Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imewataka waandishi wa habari, watangazaji na wadau wa sekta ya habari kutumia teknolojia kwa uwajibikaji ili kuhakikisha maendeleo ya kidijiti hayaathiri ubora wa habari, maadili ya taaluma na haki ya wananchi kupata taarifa sahihi. Kauli hiyo ya Bodi imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula, wakati akijibu swali la Mtangazaji Hassan Dambaya katika kipindi cha Hello Tanzania kinachorushwa na Uhuru FM, aliyetaka kujua Bodi imejiandaaje na kasi ya ukuaji wa teknolojia na matumizi ya Akili Unde inayozidi kuenea kwa kasi ikiwa na athari chanya na hasi? “Teknolojia inakwenda kasi sana na sisi lazima twende nayo hivyo hivyo kwa sababu ikituacha nyuma na sisi tutakuwa nyuma. Teknolojia hii isipotumika vizuri itakuwa na athari nyingi sana lakini ikitumika vizuri itatusaidia, sasa ni muhimu kuhakikisha haiwi mbadala wa akili zetu,” amesema Wakili Kipangula akijibu swali hilo. Amesisitiza kuwa matumi...

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU AJINYONGA MJINI BUKOBA

 Na Angela Sebastian ;Bukoba  Tukio la kusikitisha lililoacha simanzi limetokea katika shule ya Sekondari Bishop Kibira, iliyopo Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera,baada ya mwanafunzi kujinyonga. Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Blasius Chatanda, amemtaja mwanafunzi huyo kuwa Jovan Revelian Justinian, mwanafunzi wa kidato cha tatu, ambaye amekutwa amefariki baada ya kujinyonga kwa shuka ndani ya moja ya bweni shuleni hapo. Tukio hili lilitokea Juni 15, saa tisa na nusu mchana, baada ya Jovan kupatwa na msongo wa mawazo na kupotea tangu siku ya Jumapili, Juni 14 ambapo uongozi wa shule ulifanya jitihada za kumtafuta, lakini hatimaye waligundua mwili wake ukiwa umening’inia ndani ya dali la bweni, hali iliyosababisha hisia za huzuni na simanzi kwa wanafamilia, walimu, na wanafunzi.  “Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa, baadhi ya wanafunzi walibaki shuleni kwa sababu walikuwa wamepangwa na shule wapate masomo ya ziada kutokana na kutofikia wastani uliopangwa na shule katik...

MAMA NEEMA MWIGULU AHIMIZA TAASISI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUPITIA UWAJIBIKAJI KWA JAMII

 Mwenza wa Waziri Mkuu, Mama Neema Mwigulu Nchemba, amehimiza taasisi za umma na binafsi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za kijamii kupitia utekelezaji wa programu za uwajibikaji kwa jamii (CSR). Mama Neema amesema hayo leo Jumanne, Juni 16, 2026 katika hafla ya kukabidhi vifaa vya hospitali vilivyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika Hospitali ya Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya shirika hilo. Mama Neema ambae alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya kupitia ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya, ajira kwa wataalamu wa afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na kuimarisha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi. “Tunashuhudia maboresho makubwa katika sekta ya afya kutokana na uwekezaji unaoendelea kufanywa na Serikali. Leo tunajivunia huduma nyin...