Skip to main content

Posts

Showing posts from October 9, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kikwete:Waziri mkuu Majaliwa kuzindua wiki ya vijana oktoba 11,2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Ridhiwani Kikwete amesema zaidi ya Vijana 1000 wanatarajiwa kushiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa mkoani Mwanza yatakayozinduliwa Oktoba 11, 2024. Aidha, Waziri Ridhiwani Kikwete amesema Wiki hiyo huadhimishwa kila Mwaka Oktoba 8 hadi 14 kwa kuwakutanisha vijana kutoka Tanzania bara na Visiwa kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Kujadiliana, kuonesha vipaji, bunifu na kazi wanazozifanya. Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mhe. Ridhiwani amesema Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua wiki hiyo katika viwanja vya  Furahisha jijini Mwanza. Waziri Ridhiwani ametaja shughuli zitakazofanyika kwenye wiki hiyo kuwa ni pamoja na kuwapo na makongamano ya kuwajengea uelewa wa fursa za ujasiriamali, ubunifu wa kidijitali katika kujifunza na kujiajiri sambamba na elimu ya Sera mpya ya maendeleo ya vijana (2007), Toleo la Mwaka 2024. Pia, amesema kut...

Shirika la utangazaji Comoro tayari kushirikiana na Zbc na Tbc

Shirika la Utangazaji Nchini Comoro (ORTC) limeelezea utayari wake katika kushirikiana na Shirika la Utangazaji la Tanzania(TBC) pamoja na la Zanzibar(ZBC) ili kuboresha mahusiano ya kihistoria na kuendeleza lugha ya Kiswahili. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ORTC, Hablani Assoumani alipomkaribisha Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Saidi Yakubu katika makao makuu ya Shirika hilo. Bwana Hablani alimueleza Mhe. Balozi Yakubu kuwa Shirika lake lina dhamira ya kuwa na vipindi vya Kiswahili na pia kuonesha tamthilia na burudani kutoka Tanzania na ndio sababu wana makubaliano maalum na Shirika la ZBC yaliyosainiwa mwezi Julai na pia TBC ambayo yanahitaji kuhuishwa. Kwa upande wake Mhe. Balozi Yakubu alimueleza kuwa makubaliano yao na ZBC yanatoa fursa pia ya kubadilishana ujuzi na wataalamu kwa vipindi maalum na ni wakati muafaka viongozi wa juu kutembeleana kwa faida ya pande zote mbili. Katika kikao hicho, Mhe. Balozi Yakubu alipata pia fursa ya kutembelea studio kadhaa na ku...

Vijana wa UVCCM Waanza Matembezi ya Kumbukizi ya Miaka 25 ya Kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere

  Vijana 2,100 wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) kutoka Bara na Zanzibar wameanza matembezi ya siku 5 ya mshikamano, ya kilomita 200, ya kumbukizi ya miaka 25 ya kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ili kushiriki kilele cha kitaifa cha mbio za Mwenge wa Uhuru 2024. Vijana hao wameanza matembezi hayo leo kutoka Kijiji cha Mwitongo, alikozaliwa Mwalimu Julius Nyerere, kuelekea Jijini Mwanza, huku wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoani hapa, Mary Joseph. Rehema Sombi, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, amesisitiza vijana na jamii kwa ujumla kuendelea kudumisha amani iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere ili kuendelea kunufaika na matunda ya uhuru wa nchi yetu. Sombi ameiomba jamii kushiriki mchakato wa kujiandikisha na kushiriki uchaguzi, na vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mara, Mary Joseph, ametumia nafasi hiyo kuwasisitizia vijana ku...

Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani Kutumika Kutoa Elimu ya Lishe Kagera

  Na Angela Sebastian  Waziri wa kilimo Hussein Bashe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha siku ya chakula duniani Kitaifa ambayo yanatarajiwa kuanza Oktoba 10 hadi 16 mwaka huu katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.  Hayo yameelezwa na mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa wakati akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake . Aidha hajati Mwassa amesema wananchi wa mkoa wa Kagera wanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na matumizi sahii ya vyakula wanavyozalisha na badala yake huuza nje ya mkoa hari inayosababisha uwepo wa lishe duni hivyo,wanapokula chakula wanatakiwa kula chakula chenye protini ya kutosha,wanga,mafuta,matunda na mboga za majani. "Kazi kubwa katika maonesho ya siku ya chakula duniani ni kutoa elimu ya kutosha juu ya lishe ambapo kwa sasa mkoa wa Kagera tunayo asilimia 34 ya kiwango cha lishe hivyo elimu ndiyo  itakayokamilisha  maana ya siku ya chakula duniani"amesema Mwassa  Amesema kauli mbiu ya mwa...

Rais Mwinyi:Zanzibar na Comoro kuendeleza uhusiano wa kibiashara

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema wakati umefika wakurejesha diplomasia ya Uchumi na kuendeleza biashara baina ya Zanzibar na Comoro kwa maslahi ya pande zote mbili. Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo tarehe 9 Oktoba 2024, Ikulu Zanzibar alipozungumza na Gavana wa Jiji la Moroni, Visiwa vya Ngazija, Bw. Ibrahim Mzee aliyefika na ujumbe wake kuwasilisha dhamira ya kukuza ushirikiano baina nchi mbili hizo. Aidha Rais Dk. Mwinyi aliushauri ujumbe huo kurejesha makundi ya wafanyabiashara wa nchi hiyo kuja Zanzibar kuangalia fursa za biashara na uwekezaji kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Amesema, ni vema kwa pande mbili hizo kufirikia namna ya kurejesha huduma ya usafiri wa vyombo vya baharini ili kuwanufaisha wananchi wa pande mbili hizo na fursa za biasahara na kijamii zilizopo. Halikadhalika, Dk. Mwinyi alishauri ujumbe huo kuweka utaratibu maalumu kwa walimu wa Zanzibar kwenda Comoro kufundisha Kiswahili au Wakomoro kuja Zanzibar kujifunza l...

Makamu wa Rais aagiza kushughulikiwa kwa wanaohujumu sekta ya Tumbaku

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amempa rungu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, kuwashughulikia wanaohujumu sekta ya tumbaku Mkoani Tabora. Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri huyo kuwatolea uvivu wanaohujumu sekta ya tumbaku na kumueleza Makamu wa Rais kuwa jopo hilo linaongozwa na  Wafanyabiashara watumishi, wanasiasa na vingozi wa vyama vya ushirika. Akizungumza jana katika mwendelezo wa ziara yake ya siku nne mkoani Tabora Makamu wa Rais Dkt. Mpango amempa rungu Waziri Bashe kutowaonea haya wahusika na kuendelea kuwachukulia hatua. “Mimi na Rais Dkt. Samia tunakupa ridhaa Waziri wa Kilimo washughulikie na chukua hatua tupo nyuma yako, hatuwezi kuvumilia watu wanaohujumu sekta hii muhimu ya kilimo cha tumbaku. “Kampuni zisizo taka  kulipa wakulima kwa wakati pia Waziri wafutie tu leseni usirudi nyuma waone haya kuwanyonya wakulima wetu,”amesema. Makamu Mpango, amemuelekeza Waziri Bashe, kuendelea kushughulikia changamoto zilizopo katika masuala ya ruzuku kwa wakulima wa tumba...