Halmashauri ya wilaya Bariadi Mkoani Simiyu imekabidhi Majengo yaliyokuwa ya shule ya Sekondari Tarajali ya wasichana Matongo kwa wizara ya maliasili na Utalii ili yatumike kufundishia Taaluma ya wanyamapori. Makabidhiano ya Majengo hayo,Mkuu wa wilaya Bariadi Simon Simalenga amesema kuwa uwepo wa Chuo cha Taaluma ya Uhifadhi wa maliasili katika wilaya ya Bariadi kutatoa fursa kwa jamii kujifunza pamoja na kutumia mbinu za kuzuia wanyama wakali na waharibifu ikiwemo Tembo. Simalenga aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa Simiyu kwenye hafla hiyo amesema kuwa kuwepo kwa chuo cha Taaluma ya wanyamapori wilayani Bariadi pia kunatarajia kufungua fursa nyingi zikiwemo za kiuchumi na hivyo kuchochea ongezeko la mapato yatokanayo na sekta ya uhifadhi wa wanyamapori Kwa Mujibu wa Mkuu huyo wa wilaya Bariadi,Moja ya Mipa ngo ya Mkoa Simiyu ni kujenga uwanja wa Ndege ambao utatumika kuleta watalii wa Nje na ndani ili kuendeleza azma ya serikali ya kuufungua zaidi Mkoa huo. Shule hiyo yenye Jum...
Marato tv - Sauti ya Jamii