Skip to main content

Posts

Showing posts from December 9, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Misungwi yaadhimisha Miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika Kwa Kufanya Usafi wa Mazingira Kwenye Maeneo ya Umma

Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza imeadhimisha sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya umma ikiwemo Kituo cha Magazine Misungwi,Solo kuu la Misungwi na Soko la Jioni la Gwambina. Akizungumza na Wananchi na Watumishi walioshiriki kufanya usafi kati tarehe 9 Disemba 2024, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi amewataka wananchi kuendelea kufanya usafi katika maeneo yao sanjari na kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa na  kuonya kuwa watakaopuuzia zoezi la usafi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Mhe. Samizi ameongeza kuwa tangu kipindi cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere hadi hivi sasa yametendeka mengi ikiwemo Ujenzi wa Daraja la JPM, Shule za msingi na Sekondari, miradi ya maji, Vituo vya afya na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya iliyopo Iteja,  pamoja na Barabara.  Kupitia awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuna mabadiliko sana ambapo asilimia kubwa ya watu ni vijana ambao hawakushiriki haraka...

Vitendo Vya Ukatili wa Kijinsia Mkoa wa Mara Ukiwemo na Ukeketaji Vimeshuka Hadi Kufikia Asilimia 28

Fresha Kinasa- Mara WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt.  Dorothy Gwajima amesema mkoa wa Mara umeendelea kupiga hatua katika kupambana na vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ukiwemo ukeketaji ambao umeshuka  hadi asilimia  28, na kutoka nafasi ya kwanza  kama ulivyokuwa  hapo awali.   Huku mikoa ya Arusha na Manyara ikiitaja  kuongoza hapa nchini  kwa kufungana kwa  kuwa na asilimia 43.   Waziri Dkt.  Gwajima ameyasema hayo Dicemba 9, 2024, katika kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa Kijinsia Kitaifa  zilizofanyika Uwanja wa shule ya Sekondari Ingwe  Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara. Huku akisema ukeketaji umepungua kwa kiwango Cha asilimia 2 kitaifa. Ambapo wadau mbalimbali kutoka Serikalini, Mashirika ya Kiraia, Taasisi za Dini, Wazee wa Kimila, na Wananchi wameshiriki  katika kilele hicho chini ya kauli mbiu   ya mwaka huu isemayo "k...

Dkt. Mahera akutana na Mwakilishi wa Marekani Juu ya Chakula Mashuleni

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Charles Wilson Mahera (Katikati) akiwa na Mwakilishi wa Serikali ya Marekani kutoka idara ya kilimo USDA na Wawakilishi wa shirika lisilo la kiserikali Global Community la nchini Tanzania katika mkutano wa kimataifa unaojadili umuhimu wa kutoa chakula mashuleni.  Mkutano huo ni muhimu sana kwa Tanzania ambapo Tanzania imeanza kutekeleza mradi mpya kutoa chakula mashuleni awamu ya pili Mkoani Mara na Dodoma.  Awamu ya kwanza ilikuwa ni Mkoa wa Mara katika halmashauri za Musoma vijijini, Butiama, Bunda Mjini na halmashauri ya Wilaya Bunda.

Rais Mwinyi ashiriki Maziko ya Bi Mtumwa Salum

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi  amewaongoza  Viongozi na  Wananchi mbalimbali katika Maziko ya Bi Mtumwa Ali Salum , Mama mzazi wa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Othman Ame Chum. Maziko hayo yamefanyika  kijijini Kwao Mwera  Kiongoni  Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.  Awali Alhaj Dk.Mwinyi alijumuika na  Waumini wa dini ya Kiislamu  katika Sala ya  Maiti Msikiti wa Mame Ali Saateni iliyoongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih. Marehemu Bi. Mtumwa Amefariki  wakati akitibiwa  Katika Hospitali  ya Rufaa ya Lumumba  alikolazwa. Rais Alhaj Dk.Mwinyi Ijumaa ya wiki iliyopita aliwahi kumjulia hali Marehemu Bi.Mtumwa Hospitalini hapo.

Kawaida amfariji Kheri James

 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Ndugu. MOHAMMED ALI KAWAIDA (MCC) amefika Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Kumfariji Ndugu. Kheri James ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini aliyefiwa na Baba yake Mzazi Desemba 03 Mwaka huu. Mwenyekiti Kawaida akiwa Nyumbani hapo amesaini Kitabu Cha Maombelezo na kuhani msiba leo tarehe 09 Desemba 2024. *#PumzikaKwaAmani*

Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kukomesha Mauaji ya Watu Wenye Ualibino Wapongezwa

Na Hamida Ramadhan, Dodoma WADAU mbalimbali wamejitokeza kupongeza hatua ya serikali kuzindua Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki na Ustawi kwa Watu Wenye Ualbino, wakisisitiza kuwa kama utatekelezwa ipasavyo, utasaidia kukomesha mauaji na ukatili dhidi ya watu wenye ualbino nchini. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya FDH inayojihusisha na masuala ya watu wenye ulemavu mkoani Dodoma, Maiko Salali, alisema hayo hivi karibuni wakati wa kutoa tamko la kuipongeza serikali kwa kufanikisha mpango huo muhimu. "Ni imani yetu kuwa mara baada ya kuzinduliwa kwa mpango huu, changamoto nyingi zilizokuwa zikiwakabili watu wenye ualbino nchini zitapatiwa suluhisho, na kundi hili litaweza kufurahia maisha yao ndani ya taifa sawa na wananchi wengine," alisema Salali. Alibainisha kuwa watu wenye ualbino wamekuwa wakikumbwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo mitazamo hasi kutoka kwa jamii. Alisema mitazamo hiyo potofu imekuwa chanzo cha madhila makubwa, ikiwemo mauaji, kukatwa viungo, na ukatili wa a...

Rais Samia amefumua na Kulisuka Jeshi la Polisi

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya Uteuzi wa Makamishna wa Jeshi la Polisi.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.Moses Kusiluka,Makamishna Walioteuliwa ni Naibu Kamishna wa Polisi DCP.Kombo Khamis Kombo ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na Kuteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar,Kuchukua nafasi ya CP.Hamad Khamis Hamad ambaye ameteuliwa kuwa Balozi. Naibu Kamishna wa Polisi DCP.Tatu Rashid Jumbe amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na Kuteuliwa kuwa Kamishna wa Utawala na Menejiment ya Rasilimali Watu Katika Jeshi la Polisi,anachukua nafasi ya CP Suzan Kaganda ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.