Skip to main content

Posts

Showing posts from September 5, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MWENGE WA UHURU WAMULIKA FURSA MPYA ZA UCHUMI NGARA KUPITIA BARABARA YA MAGEREZA-KABALENZI.

 Na Angela Sebastian, Ngara Baadhi ya wakazi wa Kata ya Ngara mjini, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, wameeleza kuwa ujenzi wa barabara ya Magereza–Kabalenzi kwa kiwango cha lami utarahisisha usafiri na usafirishaji wa mazao kwenda sokoni, hatua wanayoamini itachochea shughuli za kiuchumi na kuongeza kipato cha wananchi pamoja na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa. Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 0.55 imejengwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Ngara kwa gharama ya zaidi ya Shilingi milioni 316. Mbali na kuboresha mandhari ya mji, wananchi wameitaja kuwa ni fursa muhimu ya kurahisisha usafirishaji wa bidhaa, ikiwemo mazao yanayopelekwa katika nchi jirani ya Burundi hivyo kuongeza mzunguko wa biashara katika eneo hilo. Meneja wa TARURA Wilaya ya Ngara, Mhandisi Mokoro Magori, akisoma taarifa ya mradi huo kwa kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa 2026a amesema mradi huo ulianza kutekelezwa Oktoba 2024 na unalenga kuboresha miundombinu ya barabara pamoj...

MWENYEKITI RAJAB ABDALLAH NA MKAKATI WA UJENZI MAKAZI KWA WATUMISHI WA CCM TANGA

NA: DK. REUBENI LUMBAGALA  Malazi, chakula na mavazi ni mahitaji ya msingi ya binadamu. Mwanadamu anapoyapata mahitaji haya kwa ukamilifu wake, hujenga utulivu wa akili, moyo na ari ya kufanya kazi kwa bidii. Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini kinatekeleza mpango mkakati wake wa kuhakikisha watumishi wa Chama wanajengewa makazi ya kudumu kwani makazi ni hitaji la msingi la binadamu. Kupatikana kwa makazi hayo, kunachochea uwajibikaji na uchapakazi wa watumishi hao, ambao wapo nchi nzima kwa madhumuni ya kuwatumikia wananchi. CCM mkoani Tanga, chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake, Rajab Abdallah, maarufu "Ustadhi Rajab," ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MCC), umedhamiria kuhakikisha ujenzi wa nyumba 36 unakamilika kwa wakati katika wilaya zote tisa za mkoa wa Tanga.  Kila wilaya zitajengwa nyumba nne za makatibu wa Chama wilaya, na za makatibu wa jumuiya ya vijana, wanawake na wazazi. Jumla ya gharama za nyumba zote 36 ni shilingi bilioni 2.5....

USHIRIKIANO WA WANANCHI,WADAU WA UTALII,TANAPA NI MUHIMU KUIMARISHA UHIFADHI.

 Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Ushirikiano wa Wadau wa utalii, wananchi na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)ni muhimu katika kuimarisha uhifadhi mlima Kilimanjaro. Kauli hii imetolewa na Viongozi mara baada kuripotiwa kuzuka moto ndani ya hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro. Septemba 5,2026 Waziri wa maliasili na Utalii,Dkt. Ashatu Kijaji(Mb) amewasili na kutembelea eneo ulipozuka moto ndani ya hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro. Lengo la kutembelea eneo hilo ni kuona hali ya eneo hilo pamoja  na hatua zinazochukuliwa kudhibiti na kuzima moto huo. Dkt. Kijaji amesema kuwa moto huo umedhibitiwa kwa asilimia 90 na shughuli za Utalii zinaendelea vizuri ndani ya hifadhi hiyo huku akitoa rai kwa wananchi wanaozunguka hifadhi za Taifa kuepuka shughuli zinazoweza kusababisha moto. "Wananchi wanapaswa kuzingatia mipaka iliyowekwa kati yao na maeneo hifadhi na kuepuka shughuli zinazoweza kusababisha moto na kupelekea kuleta athari kwa mazingira na wanyamapori ndani ya hifadhi...

WENFUREBE FOUNDATION WAREJESHA MATUMAINI KWA FAMILIA ZILIZOKATA TAMAA MULEBA

 Na Angela Sebastian ,Kagera  Familia mbili wilayani Muleba, mkoani Kagera, ambazo zilikuwa zikikabiliwa na changamoto kubwa za kiafya na hali ngumu ya maisha, zimepata mwanga mpya baada ya Taasisi ya Wenfurebe Foundation kutoa msaada wa jumla ya shilingi milioni nne kwa ajili ya matibabu.  Msaada huo umetolewa kupitia Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Simon Patrick Wenfurebe, kwa lengo la kuwasaidia wagonjwa hao kupata matibabu yaliyokuwa nje ya uwezo wao. Miongoni mwa walionufaika ni Stewart Onesmo, mkazi wa Muleba, ambaye alikuwa akikabiliwa na tatizo la kuvimba mguu na alihitaji fedha kwa ajili ya upasuaji. Stewart Onesmo alisema aliomba msaada wa shilingi laki sita, lakini baada ya kufikishiwa ombi hilo, Mkurugenzi wa Wenfurebe Foundation aliamua kumsaidia zaidi kwa kumpatia shilingi milioni moja ili aweze kugharamia matibabu na upasuaji wa mguu. Mnufaika mwingine ni Angelina Dauson, mkazi wa Kitongoji cha Kanone, Kijiji cha Kasheno, Kata ya Magata/Karutanga, ambaye mtoto ...

TANZANIA YAKABIDHI TANI 52 ZA DAWA NA VIFAA TIBA DRC KUKABILIANA NA EBOLA

 Na Shaban Juma, WAF – Kinshasa, DRC Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa msaada wa takribani tani 52 za bidhaa za afya zenye thamani ya Shilingi milioni 220 kwa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini humo. Akizungumza leo Septemba 5, 2026 jijini Kinshasa wakati wa makabidhiano ya msaada huo, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence George Samizi, kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe Mohamed Mchengerwa, amesema Tanzania imefika DRC kutimiza ahadi iliyotolewa na Serikali ya Tanzania ya kuwasilisha msaada huo mara Serikali ya DRC ilipokuwa tayari kuupokea. Dkt. Samizi amesema msaada huo unajumuisha vifaa vya kinga binafsi kwa wahudumu wa afya, vifaa tiba pamoja na bidhaa nyingine muhimu zinazohitajika katika mwitikio dhidi ya Ebola, zikiwa na lengo la kuwalinda wahudumu wa afya, kuimarisha huduma kwa wagonjwa na kusaidia kukata mnyororo wa maambukizi. Amesema ...

DKT. MWIGULU: KILA KIJIJI KUWA NA SEKONDARI*

*_▪︎ Aelekeza fedha zinazookolewa kwenye kubana matumizi zielekezwe kwenye huduma za wananchi_* *_▪︎ Aagiza magari ya kubeba wagonjwa yawe na mafuta, aonya wanaowachangisha wagonjwa_* *_▪︎ Ampongeza Afisa Elimu aliyesimamia shule kuongoza kitaifa_* WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali imejipanga kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu, ikiwemo kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na shule ya sekondari, na zaidi ya vyumba 16,000 vya madarasa vikitarajiwa kujengwa ili kukidhi ongezeko la wanafunzi. Dkt. Mwigulu amesema hayo leo, Jumamosi, Septemba 05, 2026, wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma, katika Viwanja vya Halmashauri ya Bahi, alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuwasikiliza wananchi na kushughulikia changamoto zinazowakabili. Amesema uamuzi wa kuongeza muda wa elimu ya lazima hadi kidato cha nne unaleta mahitaji makubwa ya miundombinu ya elimu, yakiwemo madarasa, maabara na maktaba. “Tunaposem...

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI ADHIMISHO LA MISA TAKATIFU YA KUWEKWA WAKFU ASKOFU MSAIDIZI JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameshiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya kuwekwa Wakfu Mhashamu Vincent Mpwaji, kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, iliyofanyika katika Viwanja vya Msimbazi Center – Dar es Salaam, leo tarehe 05 Septemba 2026. Misa hiyo, imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi, ambaye ni Askofu kiongozi katika uwekaji Wakfu, akisaidiwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya pamoja na Askofu Msaidizi Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Henry Mchamungu. Pia, Adhimisho hilo limehudhuriwa na Maaskofu kutoka Majimbo Katoliki mbalimbali nchini, Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo, Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Taasisi, Mapadre, Watawa, familia, ndugu, marafiki pamoja na waumini kutoka maeneo mbalimbali.

DKT. MWIGULU AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA JENGO LA OFISI ZA HALMASHAURI YA BAHI

 Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Jumamosi, Septemba 5, 2026, amekagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Bahi na kuweka jiwe la msingi la mradi huo, unaolenga kuboresha mazingira ya utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi. Akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Kaimu Mhandisi wa Wilaya ya Bahi, Sassoche Mtenya Maduhu, amesema jengo hilo linatarajiwa kugharimu jumla ya Sh bilioni 4.868 na litajengwa kwa awamu. Amesema hadi kufikia Agosti 30, 2025, Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ilikuwa imepokea jumla ya Sh bilioni 1 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo hilo, ambapo Sh milioni 994.546 zimetumika. Katika fedha hizo, Sh milioni 980.247 zimetumika kumlipa mkandarasi M/s Hamble Ulpan Engineering Company Limited, huku Sh milioni 14.3 zikitumika kwa ununuzi wa vyuma vilivyoagizwa kutoka Kiwanda cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi umefikia asilimia 100, ukiwa um...