Skip to main content

Posts

Showing posts from July 20, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

_DKT MWIGULU: AFRIKA IGEUZE MABADILIKO YA DUNIA KUWA FURSA ZA MAENDELEO_*

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Afrika inapaswa kutumia mabadiliko yanayoendelea katika siasa, uchumi na usalama duniani kama fursa ya kuharakisha maendeleo yake. Amesema inapaswa kufanya hivyo kwa kuimarisha uongozi wa kimkakati, kuongeza thamani ya rasilimali zake na kujenga taasisi imara zitakazolinda maslahi ya wananchi wake na kuharakisha maendeleo ya Bara la Afrika. "Afrika isiendelee kuwa uwanja wa ushindani wa mataifa makubwa. Tunapaswa kutumia nafasi yetu ya kimkakati, rasilimali tulizonazo na nguvu ya watu wetu kujiletea maendeleo yenye manufaa kwa wananchi wetu," amesema. Waziri Mkuu alisema hayo leo (Jumanne, Julai 21, 2026) alipokuwa Mzungumzaji Mkuu katika Mkutano wa Pili wa Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (National Defence College – Tanzania) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Alisema dunia inaendelea kushuhudia mabadiliko makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama yanayo...

SERIKALI NA TARI VYASHIRIKIANA KATIKA KUPAMBANA NA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU

 Na AngelaSebastian, Bukoba Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Tanzania Relief Initiative (TARI) pamoja na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi imefanikiwa kuwaokoa jumla ya wahanga 160 wa usafirishaji haramu wa binadamu katika kipindi cha Julai 2025 hadi Februari 2026. Kati ya wahanga hao, 126 waliokolewa ndani ya mipaka ya Tanzania, huku 34 wakiokolewa kutoka nje ya nchi, hatua inayodhihirisha kuimarika kwa ushirikiano wa kitaifa na kimataifa katika kupambana na uhalifu huo. Takwimu hizo zimetolewa na Afisa kutoka Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Joseph, wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa sheria mkoani Kagera. Mafunzo hayo yamewakutanisha askari wa Polisi, Maafisa Uhamiaji, Waendesha Mashtaka wa Serikali na Mahakimu, yakilenga kuwaongezea uelewa wa namna ya kutambua, kuchunguza na kushughulikia kesi za usafirishaji haramu wa binadamu...

DKT. NUMBI: LCCF 2026 NI JUKWAA MUHIMU KUPANUA FURSA ZA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI*

 📍MWANZA Mwenyekiti wa Kamati ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini kutoka Tume ya Madini, Dkt. Theresia Numbi, amesema Jukwaa la Tano la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (LCCF 2026) ni jukwaa muhimu la kuwawezesha Watanzania kuongeza ushiriki wao katika uchumi wa madini kwa kuwajengea uelewa kuhusu fursa, sheria na taratibu za utoaji wa bidhaa na huduma migodini. Dkt. Numbi ameyasema hayo leo, Julai 21, 2026, alipokuwa akizungumza mubashara kupitia kipindi cha Tuongee Asubuhi kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Star TV, akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini, CPA Venance Kasiki. Amesema LCCF 2026 inatoa nafasi kwa wadau kujifunza, kujenga mitandao na kuchangamkia fursa zinazopatikana katika sekta ya madini, hususan katika eneo la ushirikishwaji wa Watanzania katika mnyororo wa thamani wa sekta hiyo. Dkt. Numbi amesema utekelezaji wa sera ya ushirikishwaji wa Watanzania ni muhimu katika kuhakikish...

SPIKA ZUNGU AIELEZA DUNIA KUHUSU MAGARI YA UMEME TANZANIA

New York, Marekani Spika wa Bunge Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb) amesema Bunge la Tanzania limechukua hatua madhubuti za kuhimiza matumizi ya magari ya umeme pamoja na gesi. Amesema hatua hizo zimelenga kuimarisha utekelezaji wa mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Mheshimiwa Spika ameyasema hayo leo Julai 14, 2026 wakati akiwasilisha taarifa ya Bunge la Tanzania kuhusu matumizi ya Nishati Safi kwenye Jukwaa la Kibunge katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (HLPF) 2026. Mkutano huo umefanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), jijini New York, nchini Marekani. Amesema Bunge la Tanzania limepitisha marekebisho ya sera na sheria za kodi yaliyopunguza ushuru wa magari ya umeme kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 na kwamba misamaha mbalimbali ya ushuru na kodi kwa baadhi ya magari yanayotumia umeme na gesi imetolewa ili kuongeza matumizi ya usafiri rafiki kwa mazingi...

SPIKA ZUNGU AIELEZA DUNIA KUHUSU MAGARI YA UMEME TANZANIA

 New York, Marekani Spika wa Bunge Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb) amesema Bunge la Tanzania limechukua hatua madhubuti za kuhimiza matumizi ya magari ya umeme pamoja na gesi. Amesema hatua hizo zimelenga kuimarisha utekelezaji wa mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Mheshimiwa Spika ameyasema hayo leo Julai 14, 2026 wakati akiwasilisha taarifa ya Bunge la Tanzania kuhusu matumizi ya Nishati Safi kwenye Jukwaa la Kibunge katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (HLPF) 2026. Mkutano huo umefanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), jijini New York, nchini Marekani. Amesema Bunge la Tanzania limepitisha marekebisho ya sera na sheria za kodi yaliyopunguza ushuru wa magari ya umeme kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 na kwamba misamaha mbalimbali ya ushuru na kodi kwa baadhi ya magari yanayotumia umeme na gesi imetolewa ili kuongeza matumizi ya usafiri rafiki kwa ma...

RAIS SAMIA AZINDUA MELI NNE, AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA SGR, TABORA-KIGOMA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amezindua meli nne mpya za mizigo katika Ziwa Tanganyika na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Tabora hadi Kigoma, yenye urefu wa kilomita 506. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua meli hizo leo Jul 20,2026 Mkoani kigoma ambapo amesema kuwa Serikali inaendelea kujenga mfumo jumuishi wa uchukuzi nchini unaounganisha reli, bandari, barabara na viwanja vya ndege ili kupunguza gharama za usafirishaji, kuongeza ushindani wa biashara na kufungua masoko mapya. "Kigoma haitakuwa tena mwisho wa reli. Itakuwa mwanzo wa kufunguka kwa fursa za biashara na uwekezaji," amesema Rais Dkt. Samia. Ameongeza kuwa, reli ya Tabora-Kigoma, itakapokamilika, itaunganisha mkoa huo na Bandari ya Dar es Salaam pamoja na mtandao wa bandari za kisasa katika Ziwa Tanganyika, hivyo kurahisisha usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi. Rais Dkt. Samia amesema uwekezaji unaoendelea kufany...

WAZIRI KOMBO AKUTANA NA KATIBU MKUU WA OACPS, WAKAZIA MAGEUZI NA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amekutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS), Mhe. Moussa Saleh Batraki, katika mazungumzo yaliyolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na OACPS pamoja na kuharakisha utekelezaji wa ajenda ya mageuzi ndani ya Jumuiya. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 20 Julai 2026, Waziri Kombo amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuunga mkono mageuzi yanayolenga kuifanya OACPS kuwa taasisi yenye ufanisi, uwajibikaji na uwezo mkubwa wa kuhudumia nchi wanachama.  Aidha, Waziri Kombo ameeleza umuhimu wa OACPS kuwa daraja na kiungo muhimu cha kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki, pamoja na kuwa na usimamizi bora wa rasilimali na utekelezaji wenye matokeo wa programu za Jumuiya ili kuongeza imani ya nchi wanachama na washirika wa maendeleo. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa OACPS, Mhe.Batraki...

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MZEE JOSEPH BUTIKU

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema maendeleo ya kweli ya Taifa yanategemea kujenga wananchi wenye maadili, uzalendo, uwajibikaji na mshikamano, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha utawala wa sheria na taasisi za umma. "Hakuna maendeleo ya kudumu bila kujenga watu wenye maadili, uzalendo na uwajibikaji. Kama Taifa tuna kila sababu ya kuendelea kuwekeza katika kujenga tabia ya wananchi pamoja na kuimarisha taasisi zetu," amesema. Waziri Mkuu amesema hayo leo (Jumatatu, Julai 20, 2026) alipokutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo, Mzee Butiku alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake na juhudi anazoendelea kuzifanya katika kuiongoza nchi. Pia, alimpongeza Waziri Mkuu kwa mchango wake katika kumsaidia Mheshimiwa Rais kusimamia Serikali na kuhakikisha utekelezaji wa majukum...