Kutokana na tahadhari kuhusu uwezekano wa mvua kubwa za El Niño, Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limefanya marekebisho ya ratiba ya mitihani na upimaji wa kitaifa iliyokuwa ifanyike katika miezi ya Oktoba na Novemba 2026. Akizungumza leo, Ijumaa, Septemba 25, 2026, Naibu Waziri wa Elimu, Wanu Hafidh Ameir, amesema uamuzi huo umefanyika kwa lengo la kuhakikisha usalama wa wanafunzi, walimu, wasimamizi na maofisa wengine wanaohusika na uendeshaji wa mitihani. Amesema licha ya Wizara kupokea taarifa kutoka mikoa mbalimbali kuhusu maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo, imeona umuhimu wa kufanya marekebisho ya ratiba ya uendeshaji wa Upimaji na Mitihani ya Taifa kwa mwaka 2026. “Lengo la marekebisho ya ratiba ni kuhakikisha usalama wa wanafunzi, walimu, wasimamizi na maofisa wengine wanaohusika na uendeshaji wa mitihani, pamoja na kulinda mitihani, vifaa na nyaraka za mitihani iwapo mvua kubwa zitatokea mwezi Novemba 2026,” amesema. Kwa mujibu wa ...