Jamhuri ya Slovakia imeandika ukurasa mpya katika uhusiano wake na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuzindua rasmi Ofisi ya Ubalozi wake jijini Dar es Salaam, hatua inayotarajiwa kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi na maendeleo kati ya Tanzania na Sovakia. Uzinduzi huo umefanywa kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Ulaya wa Slovakia, Mheshimiwa Juraj Blanár na Mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo Juni 11,2026 . Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Ulaya wa Jamhuri ya Slovakia, Mheshimiwa Juraj Blanár, amesema ufunguzi wa Ubalozi wa Slovakia ni hatua ya kimkakati inayodhihirisha umuhimu mkubwa ambao Serikali ya Slovakia inaipa Tanzania kama mshirika wake muhimu barani Afrika. Amesema Tanzania imeendelea kuwa kitovu muhimu cha diplomasia, biashara na maendeleo katika ukanda wa Afrika Mashariki, jambo linaloifanya kuwa lango la kuimarisha ushiri...
Marato tv - Sauti ya Jamii