Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma. Manispaa ya Musoma mkoani Mara yaweka mkakati kukabiliana na uchafu wa mazingira maeneo yaliyo machafu kukabidhiwa kinyago cha fisi. Utaratibu huo umewekwa na Ofisi ya mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo wakiwemo viongozi wa Kata. October 7,2026 utoaji wa tuzo za usafi na vinyago vya fisi vimetolewa kwa makundi mbalimbali kutoka kata, mitaa na shule. Uondoshaji taka huu unafanyika katika kata zote 16 zilizopo katika Manispaa hiyo kwenye barabara, Kaya,maduka,masoko,stendi za mabasi, taasisi viwanja vya michezo na maeneo ya wazi. Katika hafla hiyo ya utoaji tuzo hizo zimehudhuriwa na mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka ambapo amesema zoezi hilo litakuwa endelevu na litakuwa linafanyika kila mwezi ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na kuweka usalama wa afya za wananchi. "Usafi unapaswa kuwa miongoni mwa vipaumbele na kila mmoja anatakiwa kuwajibika kuweka mazingira safi kuanzia mashuleni,majumba...
Marato tv - Sauti ya Jamii