Skip to main content

Posts

Showing posts from June 29, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

DKT MUNISI: PROGRAMU YA TAIFA YA UKUZAJI UJUZI YAENDELEA KUWAJENGA VIJANA

 ✅VIJANA 5,746 WANUFAIKA NCHINI Na: Mwandishi Wetu - Mwanza Serikali imeendelea kudhihirisha dhamira thabiti ya kuwawezesha vijana kiujuzi kupitia Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Dkt. Evaline Munisi amesema hayo leo Juni 29, 2026 Mwanza alipotembelea Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Sengerema FDC kwa lengo la kukagua maendeleo ya mafunzo ya Uanagenzi yanayotolewa kupitia programu hiyo. Amesema, Serikali inalenga kujenga nguvukazi yenye ujuzi, maarifa na ubunifu ili kukidhi mahitaji ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na kuongeza ushindani katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi. Dkt. Munisi alisema Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano inaendelea kutekeleza Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi kwa kushirikiana na sekta binafsi kupitia mfumo wa ubia (PPP), huku mafunzo ya uanagenzi yakichukua nafasi muhimu katika kuziba pengo la ujuzi kwa vijana.  Vile vile, amesema kuwa mfumo huo unamw...

RAIS SAMIA KUTOA TUZO ZA RAIS KWA MLIPAKODI BORA JULAI MOSI

 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, Kesho Julai mosi, 2026, anatarajiwa kutoa rasmi Tuzo za Rais kwa Walipakodi Bora kwa walipakodi waliokidhi vigezo vilivyowekwa, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mlipakodi yanayolenga kuhamasisha utamaduni wa kulipa kodi nchini na kutambua mchango wao mkubwa katika maendeleo ya taifa. Maadhimisho hayo yanaenda sambamba na kumbukumbu ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Julai 1, 1996, yakidhihirisha mafanikio ya ushirikiano uliojengwa kati ya TRA na walipakodi kwa kipindi cha miongo mitatu katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuchangia maendeleo ya sekta mbalimbali nchini. Katika kipindi hicho chote cha miaka 30, TRA imeendelea kushirikiana kwa karibu na walipakodi, huku ikiwashukuru kwa kuendelea kutekeleza wajibu wao wa kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati, jambo lililowezesha Serikali kupata rasilimali za kugharamia maendeleo ya nchi. Kaulimbiu ya maadhimisho ya miaka 30 ya...

MIAKA 30 YA TRA, YAACHA ALAMA YA UTUNZAJI MAZINGIRA KWA KUPANDA MITI 3,850 NCHINI

 NA: DK. REUBENI LUMBAGALA, TANGA Suala la utunzaji mazingira ni la muhimu kutokana na umuhimu wake kijamii, kimazingira na kiuchumi. Mwanadamu ambaye ni sehemu ya mazingira anapaswa kuhakikisha anayatunza ili kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri na salama kwa kuishi. Katika miaka ya hivi karibuni, kumetokea majanga katika mazingira. Binadamu amekuwa akiharibu mazingira, hali inayochangia mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo mbalimbali duniani.  Mathalani, mabadiliko hayo yamesababisha upungufu wa mvua katika maeneo mbalimbali na hivyo kusababisha upungufu wa chakula hasa katika maeneo yanayotegemea kilimo cha mvua. Kutokana na madhara ya uharibifu wa mazingira, juhudi zimekuwa zikichukuliwa na serikali, mashirika, taasisi na wadau mbalimbali kuhakikisha madhara hayo yanapungua kama si kumalizika kabisa kwa kuhakikisha mazingira yanatunzwa likiwemo suala la upandaji miti katika sehemu mbalimbali. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeamua kuwa sehemu ya utunzaji mazingira nchini. ...

BOMBA LA MAFUTA CHONGOLEANI- HOIMA LAFIKIA ASILIMIA 90

 📍Mkandarasi wa umeme apewa mkwara mzito kukamilisha njia maalum ya Majani Mapana hadi Chongoleani ifikapo Agosti Na MASHAKA MHANDO, Tanga  WAZIRI wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amempa miezi miwili (hadi mwezi Agosti mwaka huu) mkandarasi anayetekeleza mradi wa umeme chini ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuhakikisha anakamilisha njia maalum (*line*) ya kufikisha nishati ya uhakika katika eneo la mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) Chongoleani jijini Tanga. Onyo hilo limetolewa leo na Waziri Ndejembi wakati wa ziara yake maalum ya kukagua maendeleo ya mradi huo wa kimkakati, ambapo alibainisha kuwa ingawa kwa sasa umeme upo, Serikali inajenga miundombinu hiyo ya dharura kutoka kituo kikubwa cha kupoza umeme cha Majani Mapana ili kuzuia changamoto za nishati mradi utakapoanza kazi. Waziri Ndejembi alisisitiza kuwa kasi ya ujenzi wa mradi huo hairuhusu kusuasua kwa sekta ya nishati, kwani mafuta ghafi yanatarajiwa kuanza kuwasili Tanga mapem...

DMG NAMED BEST MARITIME COMPANY AT MOROGORO AWARDS 2026

 By Prosper Makene Morogoro, Tanzania – June 27, 2026. Dar es Salaam Merchant Group (DMG) has clinched the coveted _Best Maritime Technology Company of the Year_ award at the 2026 Morogoro Business Awards, cementing its position as a leader in Tanzania’s technological transformation of the blue economy. The win comes just weeks after DMG was recognized by Forbes Africa as one of the few class one maritime companies in building ships in Africa, citing its pioneering work in port digitalization, shipbuilding, and smart logistics. The prestigious award was presented by Hon. Adam Kigoma Malima, Morogoro Regional Commissioner, during a gala ceremony held on June 27, 2026. The event brought together top CEOs, innovators, and government officials to celebrate enterprises driving Tanzania’s economic growth through technology and innovation. The award recognizes DMG’s commitment to _Building Dreams with Lasting Quality_ through a unified service ecosystem that spans the entire project lifec...

RC CHALAMILA ATAKA MWAROBAINI WA FOLENI DAR UPATIKANE

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amefanya kikao kazi na wadau mbalimbali wa usafirishaji na kuelekeza kuundwa kwa kamati maalumu ya kuratibu kwa haraka namna ya kushughulikia changamoto ya foleni au msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam ambapo kamati hiyo itaratibiwa na katibu Tawala wa Mkoa huo Ndg Abdul Mhinte lengo likiwa ni kupunguza au kumaliza kero hiyo.  Akizungumza Jijini Dar es Salaam mara baada ya kikao kazi hicho kilichokutanisha wadau mbalimbali ikiwemo LATRA, Mamlaka ya bandari, kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, Viongozi wa madereva malori na daladala pamoja na uwakilishi kutoka Mkoa wa Pwani, hivyo Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amesema ukuaji wa bandari ya Dar es Salaam pamoja na uhitaji wa bandari kavu eneo la jirani na bandari ni miongoni mwa mambo yanayochangia msongamano wa magari katikati ya Jiji hilo, hivyo timu hiyo itashauri namna bora ya kumaliza changamoto hizo RC Chalamila ameongeza kuwa uwepo wa mizani ya kupimia magari ...

KAMPUNI YA UTENGENEZAJI MELI YA DMG YATAJWA KAMPUNI BORA KATIKA TUZO ZA MOROGORO 2026

 Na Mwandishi Wetu  Morogoro, Tanzania – Juni 27, 2026—Kampuni ya Dar es Salaam Merchant Group (DMG) imeendelea kupokea tuzo mbalimbali za kitaifa na kimataifa zinazotambua ubora wake katika utengenezaji na ukarabati wa meli nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa na hivyo kuleta chachu ya kusukuma mbele MAENDELEO kwenye eneo la uchumi wa bluu.. Tuzo hiyo yenye heshima kubwa ilikabidhiwa Katika usiku wa tuzo maalumu za Biashara Morogoro 2026 na Mhe. Adam Kigoma Malima, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, katika hafla ya sherehe iliyofanyika Juni 27, 2026.  Tukio hilo liliwaleta pamoja wakurugenzi wakuu, wavumbuzi, na maafisa wa serikali kusherehekea mashirika yanayoendesha ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupitia teknolojia na ubunifu. Kampuni DMG iliibuka kinara kwa kuwa Kampuni mahili kwenye eneo la teknolojia za utengenezaji meli na mabadiliko kwenye uchumi wa bluu Ushindi huo wa DMG umekuja wiki chache tu baada ya Kampuni hiyo kutambuliwa na Forbes Africa kama moja ya kampuni chac...

NDEJEMBI ATOA MAAGIZO MAZITO KWA MKANDARASI WA MRADI WA UMEME TANGA

 Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga  Waziri wa nishati Mh. Deogratius Ndejembi amemtaka mkandarasi aneyetekeleza ujenzi wa njia ya umeme utakao tumika katika uendeshaji wa mitambo kuhakikisha anakamilisha kazi hiyomwanzoni mwa mwezi wa nane. Agizo hilo amelitoa akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tanga alipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Africa mashariki (EACOP) katika eneo la chongoleani ambapo mpaka sasa mradi umefikia 87% ya ujenzi. Waziri Ndejembi pia amewataka wananchi kuchangamkia fursa zitokanazo na mradi huo,huku ikionekana kwa kiasi kikubwa mradi umeitoa ajira hasa Kwa watanzania, watanzania wakionekana kuwa asilimia 84 na huku asilimia 30 ikiwa ni wakazi wa chongoleani. "Watanzania niwaombe kuulinda mradi huu kwani ni mradi mkubwa sana kiuchumi na umechangia katika ukuzaji uchumi Kwa jiji la Tanga kwani umeweza kutoa ajira na kuwapatia ujuzivijana wa kitanzania,ujazi ambao wanaweza kutumia katika ujenzi wa miradi migine kama hii", ...

OWM YASISITIZA UJUMUISHWAJI WA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA MIPANGO YA TAIFA

 Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam SERIKALI imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kuhakikisha Watu Wenye Ulemavu wanapata nafasi sawa katika nyanja zote za maendeleo, ikiwa ni pamoja na kijamii, kiuchumi na kisiasa, kupitia sera, sheria na mipango jumuishi inayotekelezwa nchini. Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Dkt. Jim Yonazi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kilichowakutanisha viongozi wa vyama vya Watu Wenye Ulemavu na mashirika yasiyo ya kiserikali kujadili utekelezaji wa sera, sheria na miongozo ya ujumuishaji nchini. Amesema hatua kubwa zimeendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha hakuna mwananchi anayeachwa nyuma, ambapo Sera ya Taifa ya Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004 pamoja na Sheria Na. 9 ya mwaka 2010 zimekuwa msingi muhimu wa utekelezaji wa haki na usawa kwa kundi hilo. “Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa kila sera, mpango na huduma inayotekelezwa nchini inazingatia ujumuishaji wa Watu Wenye Ulemavu tangu ha...

INADES-FORMATION TANZANIA YASHIRIKIANA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS KUANDAA MPANGO WA MAZINGIRA WILAYA YA BAHI

  By Prosper Makene  Katika juhudi za kuhakikisha Tanzania inafikia azma ya kuwa nchi ya kijani ifikapo mwaka 2050, Shirika la INADES-Formation Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais – Idara ya Mazingira limeandaa kikao kazi cha kuandaa Mpango wa Usimamizi wa Mazingira wa Wilaya ya Bahi, kwa kushirikisha wataalamu kutoka Wilaya za Chemba na Kondoa. Akifungua kikao hicho Leo katika ofisi ya Makamu wa Rais, Mtumba mjini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais – Idara ya Mazingira, Dk. Paul Deogratius, alisema ushiriki wa Wilaya za Chemba na Kondoa utasaidia kubadilishana uzoefu katika mchakato wa kuandaa mpango huo kwa Wilaya ya Bahi. Alieleza kuwa mipango ya usimamizi wa mazingira katika ngazi ya wilaya ni takwa la kisheria na ni nyenzo muhimu katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za mazingira zinazozikabili halmashauri nchini. "Kitaifa, zimetambuliwa zaidi ya changamoto 13 za mazingira, huku kila wilaya ikiwa na changamoto zake ...

VICE PRESIDENT'S OFFICE, INADES-FORMATION COLLABORATE ON ENVIRONMENTAL PLAN FOR BAHI DISTRICT

 By Prosper Makene  Dodoma – In efforts to ensure Tanzania achieves its goal of becoming a green country by 2050, INADES-Formation Tanzania, in collaboration with the Vice President's Office – Department of Environment, has organized a working session to develop the Bahi District Environmental Management Plan, involving experts from Chemba and Kondoa districts. Opening the session today at the Vice President's Office in Mtumba, Dodoma, the Acting Director of Environment from the Vice President's Office – Department of Environment, Dr. Paul Deogratius, said the participation of Chemba and Kondoa districts will help facilitate the exchange of experience in the process of developing the plan for Bahi District. He explained that environmental management plans at the district level are a legal requirement and are a crucial tool in addressing various environmental challenges facing local councils across the country. "Nationally, more than 13 environmental challenges have bee...

CRDB YAWEKA AFYA YA WAFANYAKAZI KIPAUMBELE ,YAAMINI USTAWI NDIYO MSINGI WA MAFANIKIO

 CRDB Bank imeendelea kuthibitisha kuwa rasilimali muhimu zaidi katika mafanikio ya taasisi ni watu wake, kwa kuendesha programu ya Wellness Day inayolenga kuimarisha afya ya mwili, akili na ustawi wa wafanyakazi, hatua inayotajwa kuwa sehemu ya mkakati wa kujenga nguvu kazi yenye tija, ubunifu na ufanisi. Akizungumza leo jijini Dodoma wakati wa programu hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CRDB, Edward Mpina, amesema benki hiyo inaamini kuwa mafanikio ya biashara hayawezi kutenganishwa na afya ya wafanyakazi wake, ndiyo maana imeendelea kuwekeza katika mipango inayowalinda na kuwajengea mazingira bora ya kufanya kazi. Mpina amesema dhana ya wellness ni pana zaidi kuliko kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza, kwani inajumuisha afya ya akili, ustawi wa kihisia, uwezo wa kukabiliana na changamoto za kazi na maisha pamoja na kujenga usawa kati ya kazi na familia. Ameeleza kuwa katika mazingira ya kisasa ya kazi, wafanyakazi hukabiliwa na shinikizo la kufikia malengo ya biashara, kutimiza via...