Skip to main content

Posts

Showing posts from October 8, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

IGUWASA YAWEKA MIKAKATI KUKABILIANA NA MVUA ZA EL-NINO IGUNGA

Na Mwandishi Wetu – Tabora MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Igunga Mjini (IGUWASA), imeweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El-Nino zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni, ikiwemo kuimarisha miundombinu ya mabomba ya maji katika maeneo hatarishi. Hatua hiyo inahusisha kuweka kingo za udongo katika maeneo yanayopitiwa na mabomba ya maji, pamoja na kuandaa vifaa vya dharura vitakavyotumika endapo kutatokea uharibifu wa miundombinu kutokana na mvua hizo. Mkurugenzi Mtendaji wa IGUWASA, Alexander Ntonge, amesema maandalizi hayo yanalenga kuhakikisha huduma ya maji inaendelea kupatikana kwa wananchi hata wakati wa mvua hizo. Ntonge pia amewataka wananchi kuchukua tahadhari, ikiwemo kuhifadhi maji ya kutosha kabla na wakati wa mvua hizo, pamoja na kutumia maji safi na salama ili kuepuka magonjwa ya mlipuko. Amesema wananchi wanapaswa kutoa taarifa haraka wanapoona uharibifu wa miundombinu ya maji, ili hatua za kurekebisha ziweze...

RAIS SAMIA APELEKA TABASAMU KWA WASANII TOZO ZIKIPUNGUZWA

Na Mwandishi Wetu Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetangaza marekebisho ya kanuni ambazo zimepunguza utitiri wa tozo na kupunguza kwa kiwango kikubwa kiwango cha ada walizokuwa wakitozwa wasanii na wanaofanya shughuli za sanaa kwa mwaka. Hayo yalitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Edward Buganga wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu marekebisho hayo ya kanuni. Alisema marekebisho ya tozo hizo kwa mwaka 2026 yalifanywa na Bunge zinazolenga kuimarisha usimamizi wa Sanaa, kuwawezesha wasanii na wadau wa Sanaa, na kupunguza utitiri wa tozo. Alisema kanuni hizi ambazo tayari zimeanza kutumika na tunawakumbusha wadaua kuwa hazilengi kuzuia ubunifu na zinaweka utaratibu unaolinda wasanii, hadhira, watoto, urithi wa Sanaa na maslahi ya wadau, huku ikiwezesha sekta kukua na kushindana ndani na nje ya nchi.  Alisema mabadiliko hayo ya kanuni yanahusu wasanii na vikundi vya Sanaa, maDJs, washereheshaji, maproduza, Mameneja,...