• Yalenga uzalishaji wa cathode ya asilimia 99 📍Kilimanjaro MKAKATI wa uongezaji thamani katika Sekta ya Madini umeanza kuzaa matunda mkoani Kilimanjaro, baada ya kampuni ya Mega Copper Co Ltd kujikita katika uongezaji wa kiwango cha ubora wa madini ya shaba kutoka asilimia moja hadi kufikia kati ya asilimia 20 na 25. Akizungumza katika kijiji cha Kiruru, wilayani Mwanga, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Ally Ng’anzo, amesema maboresho hayo yameongeza ushindani wa kampuni katika soko la kimataifa, huku China ikiwa soko kuu la sasa la mauzo ya madini hayo. Amesema pamoja na kampuni kufikia hatua hiyo ya uongezaji thamani ili kuzalisha makinikia ya shaba, matarajio yao ni kufanya uwekezaji zaidi kwa kufunga mitambo maalum ya uongezaji thamani, ili kufikia ubora wa hadi asilimia 99. Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza thamani ya bidhaa hiyo, kupanua wigo wa masoko na kuimarisha upatikanaji wa malighafi ya kutengeneza bidhaa za shaba kwa viwanda vya ndani. Kwa mujibu wa Ng’anzo, kampuni hiyo i...
Marato tv - Sauti ya Jamii