Skip to main content

Posts

Showing posts from October 31, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

RAIS JOÃO LOURENÇO WA ANGOLA AHITIMISHA ZIARA YA KITAIFA, AONDOKA NCHINI

  Akiwa jijini Dodoma, Rais Lourenço alishiriki hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba pamoja na miundombinu ya barabara zake. Mheshimiwa Lourenço aliagwa rasmi na mwenyeji wake Rais Samia katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma kabla ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Dodoma. Katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma Mheshimiwa Lourenço alisindikizwa na kuagwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb.) Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Balozi wa Tanzania anayewakilisha Angola mwenye makazi yake Zambia Injinia Cyprian Luhemeja, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Angola Bw. Mbwana Mziray na viongozi wengine wa Serikali.

WANANCHI IGUNGA WAHAIDI KUJIUNGA NA HUDUMA YA UMEME NA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

  *WANANCHI IGUNGA WAHAIDI KUJIUNGA NA HUDUMA YA UMEME NA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA* 📌 *Sasa Umeme ni Kitongoji kwa Kitongoji* 📌 *Nishati Safi ya Kupikia kwa Kila Mtanzania* 📍 *Igunga, Tabora* Wananchi wa vijiji vya Maguguni, Lubeho na Mwama Bogo, Wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora, wameahidi kujiunga na huduma ya umeme na kuanza kutumia nishati safi ya kupikia baada ya kupatiwa elimu kuhusu umuhimu na manufaa ya matumizi ya nishati hizo na wataalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Ahadi hizo zimetolewa kufuatia ziara ya wataalam wa REA waliotembelea vijiji hivyo na kufanya mikutano na wananchi kwa lengo la kutoa elimu na kuhamasisha matumizi ya umeme pamoja na nishati safi ya kupikia, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuboresha upatikanaji na matumizi ya nishati bora kwa wananchi waishio vijijini. Kupitia mikutano hiyo, wananchi wamepata fursa ya kuelewa manufaa mbalimbali yatokanayo na upatikanaji na matumizi ya umeme, yakiwemo kukuza shughuli za kiuchumi, k...

INEC YAWAPA NENO MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA KATA YA NONDE

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka Makarani Waongozaji Wapiga Kura katika kata ya Nonde iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya kutekeleza majukumu yao kwa weledi.   Hayo yamebainishwa leo Oktoba 31, 2026 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele wakati akizungumza na watendaji hao alipotembelea mafunzo yao ya siku moja ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata ya Nonde unaotarajiwa kufanyika tarehe 04 Novemba,2026.   Jaji Mwambegele  amewasisitiza washiriki hao  kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni ili kuufanya uchaguzi huo kuwa huru na wa haki.   Awali kabla ya ufunguzi wa Mafunzo haya, washiriki hao waliapa kiapo cha kutunza siri na kile cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa haki na weledi.   Uchaguzi huo utafanyika ikiwa ni miongoni mwa kata  kata 11 za Tanzania Bara ambazo ni Lugenge, Halma...

POLISI NA MABALOZI WA USALAMA BARABARANI DODOMA WATOA ELIMU KWA WANANCHI

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, kwa kushirikiana na mabalozi wa usalama barabarani limeendelea kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani. Akizungumza leo Oktoba 31,2026 katika kampeni hiyo, Afisa kutoka kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Dodoma kitengo cha elimu SGT Ester Makalo amesisitiza kuwa watembea kwa miguu wana haki ya kutumia vivuko vya waenda kwa miguu muda wote mchana na usiku na kwamba madereva wanapaswa kuwapa nafasi wanapotaka kuvuka barabara. Amesema kila mtumiaji wa barabara ana wajibu wa kuhakikisha usalama wake na wa wengine, akiwataka madereva kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani. “Familia zetu zinatusubiri nyumbani, tunataka kila mmoja wetu awe balozi wa usalama barabarani na kusaidia kujenga utamaduni wa matumizi sahihi ya barabara,” amesema. Aidha, ametoa wito kwa watumiaji wa barabara kuwa makini katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka, amba...