Skip to main content

Posts

Showing posts from September 15, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Amwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Katika Baraza la Maulid

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 16, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Baraza la Maulid yanayofanyika kitaifa mkoani Geita kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu.

Je Unafahamu Kuwa Unaweza Kutumia Pump za Umwagiliaji Zinazotumia Solar Zinazohamishika Kumwagilia Shamba Zaidi ya Moja Kwa Gharama Nafuu?

  Na Emmanuel Chibasa Katika maeneo ya vijijini mkoani Mara, wakulima wanakumbana na changamoto katika kilimo Cha umwagiliaji kutokana na kukosa elimu ya matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kutengeneza mifumo ya nishati ya jua (Solar) unaohamishika Ili kupunguza gharama za uendeshaji wanazotumia Katika pump za mafuta. Uchunguzi uliofanywa George Marato Tv katika baadhi ya maeneo Musoma umebaini kuwa  wakulima wanatumia pamp za mafuta ambazo wanaweza kumwagilia Kwa kuhamisha lakini hawana uelewa kuwa Kuna teknolojia ya mfumo wa pump za umwagiliaji Zinazotumia solar zinazohamishika na hivyo kuwa ni Suluhu mbadala ya kupunguza gharama wanazotumia Katika pump za mafuta lakini pia kuhifadhi mazao baada ya mavuno Ili yasiharibike. Wakulima pia hawana uelewa wa kutosha juu ya matumizi ya Teknolojia ya umeme jua inauwezo WA Kuongeza uzalishaji na kupunguza upotevu WA mazao baada ya mavuno na Kuboresha Maisha ya wakulima na Uchumi wa nchi Kwa ujumla na teknolojia hii inaweza Kuleta...

Waziri Nchemba ajivunia mafanikio ya serikali katika ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya elimu

  Serikali imekamilisha ujenzi wa Taasisi ya uhasibu Tanzania(TIA)kampasi ya Nyang'homango mkoani mwanza ili kusogeza huduma ya elimu kwa wananchi wa kanda ya ziwa Waziri wa fedha Dkt.Mwigulu Nchemba amekagua ujenzi wa Taasisi hiyo na kueleza kuridhishwa na matumizi ya shilingi billioni 7.3 zilizotumika kugharamia ujenzi huo.  Nchemba amesema kuwa uwepo wa Taasisi hiyo utachochea ongezeko la shughuli za kiuchumi katika eneo la Nyang'omango na kata ya usagara kwa ujumla na kuwaasa wananchi kutumia fursa ya chuo hicho kubuni miradi ya kujikwamua kiuchumi.  Waziri Nchemba amesema kuwa ujenzi wa Taasisi hiyo ni mkakati wa serikali wa kujenga miundombinu bora ya elimu ili kuimarisha mazingira ya kujifunza na kufundishia.  "Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuwaletea watanzania maendeleo katika kipindi cha miaka mitatu ambayo imegusa nyanja zote ikiwemo elimu na afya,hakuna eneo lolote nchi hii ambayo haijanufaika na miradi mathalani ya elimu"alisema Nchemba ...

Wazazi na Walezi Watakiwa Kuwalea Watoto Kimaadili na Kudhibiti Matumizi ya Simu

Wazazi na walezi wametakiwa kuwalea watoto wao kwa kuzingatia maadili mema na kuhakikisha wanadhibiti matumizi ya simu na teknolojia nyingine, ambazo zinatajwa kuwa na madhara makubwa endapo zitatumiwa bila udhibiti. Akizungumza wakati wa mahafali ya 12 ya Shule ya Msingi Waja, Mkurugenzi wa Makampuni ya Waja, Chacha Wambura, alisema kuwa ni jukumu la wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanapata malezi bora yanayowajenga kuwa raia wema.  Ameongeza kuwa matumizi mabaya ya simu na teknolojia, hasa mitandao ya kijamii, yanaweza kuwa chanzo cha tabia zisizofaa miongoni mwa watoto. “Mazingira ya sasa yanahitaji wazazi kuwa makini zaidi. Tunapaswa kuwaelekeza watoto wetu matumizi sahihi ya teknolojia ili kuepuka madhara yanayoweza kusababisha athari mbaya kwa ukuaji wao,” alisema Chacha Wambura. Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati, ameeleza kuwa shule za Waja zimeendelea kuwa mfano mzuri katika kutoa elimu bora na kuwalea watoto katika mising...

Masauni Akutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa Quatar Nchini Tanzania

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini Tanzania,Fahad Rashid Al Murikhi(kushoto).Mazungumzo hayo yaliyohusu ushirikiano wa nchi hizo mbili katika kuimarisha masuala ya Ulinzi na Usalama yamefanyika Makao Makuu ndogo ya wizara hiyo,jijini Dar es Salaam.

Wizara ya Madini yavunja rekodi ukusanyaji wa maduhuli

  Ndani ya miezi miwili yakusanya shilingi bilioni196 ikiwa ni zaidi ya kiasi kilichokusanywa katika mwaka wa fedha 2015/2016 cha shilingi bilioni 161 Waziri Mavunde apongeza Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kwa kuibeba Sekta ya Madini kupitia ukusanyaji wa maduhuli. Ampongeza Rais Samia kwa kuipa kipaumbele Sekta ya Madini kwa kuongeza bajeti kwa mwaka 2024/2025 Atoa maagizo matano kwa Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa TANGA. Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amepongeza maafisa madini wakazi wa mikoa kwa kuvunja rekodi ya kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 196 kwa kipindi cha miezi miwili katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025 kiasi ambacho ni zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 161 kilichokusanywa kwa mwaka mzima wa fedha 2015/2016. Mhe. Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Septemba 15, 2024 kupitia kikao chake na menejimenti ya Tume ya Madini ikiwa ni pamoja na wakurugenzi, mameneja na maafisa madini wakazi wa mikoa chenye lengo la kuweka mikakati ya kuimarisha Sekta ya Ma...

Wizara ya Madini yakusanya Bilioni 196 kwa miezi miwili

Ndani ya miezi miwili yakusanya shilingi bilioni196 ikiwa ni zaidi ya kiasi kilichokusanywa katika mwaka wa fedha 2015/2016 cha shilingi bilioni 161 Waziri Mavunde apongeza Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kwa kuibeba Sekta ya Madini kupitia ukusanyaji wa maduhuli. Ampongeza Rais Samia kwa kuipa kipaumbele Sekta ya Madini kwa kuongeza bajeti kwa mwaka 2024/2025 Atoa maagizo matano kwa Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amepongeza maafisa madini wakazi wa mikoa kwa kuvunja rekodi ya kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 196 kwa kipindi cha miezi miwili katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025 kiasi ambacho ni zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 161 kilichokusanywa kwa mwaka mzima wa fedha 2015/2016. Mhe. Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Septemba 15, 2024 kupitia kikao chake na menejimenti ya Tume ya Madini ikiwa ni pamoja na wakurugenzi, mameneja na maafisa madini wakazi wa mikoa chenye lengo la kuweka mikakati ya kuimarisha Sekta ya Madini katika k...