Skip to main content

Posts

Showing posts from May 6, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tanzania Kufanya Mageuzi Makubwa Sekta Ya Ardhi-Ndejembi

SERIKALI ya Tanzania imetangaza mageuzi makubwa ya sekta ya ardhi yanayolenga kuboresha usimamizi, kuchochea ukuaji wa uchumi, na kulinda haki za wananchi wake.  Akizungumza katika siku ya pili Mkutano wa Kimataifa wa Sekta ya Ardhi ulioandaliwa na Benki ya Dunia katika Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Washington DC, Marekani Mei 06, 2025, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amesema mageuzi hayo yamefanywa na Serikali kupitia Sera ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995 (Toleo la Mwaka 2023) ambayo ilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Machi 17, 2025 jijini Dodoma. Waziri Ndejembi amesema Sera hiyo inalenga kuboresha usimamizi wa ardhi kwa kuweka msingi imara wa haki, usawa na matumizi endelevu ya rasilimali hiyo muhimu.  ‘‘Mageuzi haya yanatokana na uhitaji unaoendana na mahitaji ya sasa ya kijamii na kiuchumi, pamoja na kukabiliana na changamoto kama migogoro ya ardhi, ukuaji wa mijini na mabadiliko ...

Waziri Mavunde Atangaza Kiama Kwa Kampuni 95 za Uchimbaji Madini

   ▪️Yatoa hati za makosa kwa kukiuka masharti ya Leseni ▪️Kampuni 7 tu kati ya 95 ambazo hazijaanza uchimbaji zimelaza mtaji wa Trilion 15  ▪️Zapewa siku 30 kujibu hoja *Dar Es Salaam* SERIKALI  imetoa Hati za Makosa kwa Kampuni  95 za Uchimbaji Mkubwa na wa Kati wa Madini kutokana na wamiliki wa leseni hizo kukiuka masharti ya Leseni  kama yalivyoainishwa kwenye Sheria ya Madini. Akizungumza leo Mei 6, 2025 jijiini Dar es Salaam, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amesema kampuni hizo zinapaswa kujibu hoja ndani ya siku 30 la sivyo zitafutiwa leseni zao. Hati hizo za makosa zimetolewa rasmi kuanzia Aprili 14, 2025 na muda wake utamalizika Mei 13 mwaka huu.   “Kama wanahoja walete majibu yao, tuyahakiki tukijiridhisha na hoja zao tutawaondolea makatazo kama hawana hoja tutawafutia leseni zao kwa  mujibu wa Sheria ya Madini Sura 123  ya  utoaji na ufutaji wa leseni za  madini na uchimbaji kifungu cha 63 na Kanuni zake, amba...