Skip to main content

Posts

Showing posts from August 23, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

DKT. NYANSAHO: KITUO CHA FORODHA MANYOVU KUONGEZA MAPATO NA KUIMARISHA USALAMA

 WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho, amesema ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha Manyovu, kilichopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, ni hatua muhimu katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali, kurahisisha huduma za forodha pamoja na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa shughuli za mpakani. Dkt. Nyansaho ameyasema hayo wakati wa ziara yake mkoani Kigoma, ambapo amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo ya kimkakati, ikiwemo Kituo cha Pamoja cha Forodha Manyovu na ujenzi wa Barabara ya Kabingo–Kasulu Manyovu. Amesema kukamilika kwa kituo hicho kutakuwa na manufaa makubwa kwa Serikali na wananchi kwa kuwa kitaweka pamoja huduma mbalimbali zinazohusiana na shughuli za forodha, hivyo kupunguza usumbufu na kurahisisha utoaji wa huduma kwa watu wanaotumia mpaka huo. Waziri Nyansaho, amesema uwepo wa kituo hicho unatarajiwa pia kuongeza ufanisi katika udhibiti wa shughuli zinazofanyika mpakani, sambamba na kuhakikisha Serikali inapata mapato yanay...

MAGANYA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MEATU, ATOA MSUKUMO KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Ndugu Fadhili Rajabu Maganya, ameendelea na ziara yake Wilayani Meatu, Mkoa wa Simiyu, kwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu, akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyokusudiwa. Katika ziara hiyo, Mwenyekiti Maganya ameambatana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndugu Shamsa Mohamed, pamoja na viongozi na watendaji mbalimbali. Akiwa Shule ya Msingi Meatu, Mwenyekiti Maganya amekagua ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa wenye thamani ya Shilingi milioni 125, unaolenga kuongeza nafasi za kujifunzia na kuweka mazingira bora kwa wanafunzi na walimu. Aidha, ametembelea Shule ya Sekondari Meatu, ambako amekagua miundombinu ya shule hiyo na kupata taarifa kuhusu maendeleo pamoja na hali ya mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Katika ziara hiyo, Mwenyekiti Maganya pia ametembelea mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Wazazi Wilaya ya Meatu pamoja na ...

BALOZI KHAMIS OMAR AALIKWA MAZUNGUMZO YA UFADHILI ENDELEVU WA AFYA AFRIKA

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amewasili Addis Ababa, Ethiopia, kushiriki kama mwanajopo katika Mazungumzo ya Mawaziri wa Fedha kuhusu ufadhili endelevu wa afya barani Afrika katika kipindi cha ufinyu wa bajeti na juhudi za nchi kujitegemea katika masuala ya afya. Mhe. Omar amepokea taarifa kuhusu maandalizi ya ushiriki wake na agenda za mkutano huo kutoka kwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia. Mazungumzo hayo yanawakutanisha Mawaziri wa Afya na Fedha, washirika wa maendeleo na viongozi wa kikanda kujadili changamoto za kifedha zinazoathiri upatikanaji wa huduma za afya kwa wote (UHC), ikiwemo kupungua kwa misaada kutoka nje, ufinyu wa bajeti na kuongezeka kwa mzigo wa madeni. Mkutano huo unafanyika kabla ya Kikao cha 76 cha Kamati ya Kanda ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa Afrika.

RAIS MUSEVENI AWAASA MAAFISA WASTAAFU KUTUMIA BUSARA MAFAO YAO

 Rais wa Uganda na Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF), Yoweri Kaguta Museveni, amewaaga rasmi maafisa wakuu 19 wa jeshi hilo waliostaafu, akiwataka kutumia kwa busara mafao na akiba zao ili kujenga maisha salama na yenye uhakika wa kifedha baada ya utumishi. Akizungumza katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Entebbe, Rais Museveni amewapongeza maafisa hao kwa miaka yao ya utumishi na mchango wao katika kujenga na kuimarisha UPDF pamoja na kulinda amani na usalama wa Uganda. Amewataka wastaafu hao kuepuka kufanya maamuzi ya haraka katika matumizi ya mafao yao, badala yake kuelekeza fedha katika uwekezaji salama na wenye uwezo wa kuzalisha kipato cha kudumu. Museveni ametaja uwekezaji katika hati fungani za Serikali kuwa miongoni mwa maeneo salama, akieleza kuwa unaweza kumwezesha mstaafu kupata mapato ya riba bila kulazimika kushiriki moja kwa moja katika uendeshaji wa biashara. “Ukiweka Shilingi milioni 600 na ukapata asilimia 15, mwishoni mwa mwaka hiyo n...

WANAFUNZI 95 WAENDA INDIA KUSOMEA AI, UHANDISI

 Na Mwandishi Wetu Zaidi ya wanafunzi 95 wa Kitanzania wameondoka nchini kuelekea India kuanza masomo ya elimu ya juu katika vyuo mbalimbali, ikiwa ni kundi la kwanza kati ya wanafunzi 198 wanaotarajiwa kwenda kusoma nchini humo kupitia Global Education Link katika mwaka 2026. Wanafunzi hao walioondoka kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Terminal 3, jijini Dar es Salaam, wengi wao wamechagua programu zinazohusiana na sayansi, teknolojia na taaluma zinazohitajika katika dunia ya sasa, zikiwemo Computer Engineering, Cyber Security, Artificial Intelligence, Civil Engineering, programu mbalimbali za afya, sheria na biashara. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Meneja wa Tawi la Dar es Salaam, Micky Musa, amesema kuondoka kwa wanafunzi hao ni sehemu ya mpango mpana wa kuwaunganisha vijana wa Tanzania na fursa za elimu ya kimataifa. “Zaidi ya wanafunzi 95 wanaondoka katika kundi hili la kwanza kuelekea India, lakini kwa mwaka huu tun...

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA MWANANYAMALA

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amefanya ziara ya kushtukiza leo Jumapili, Agosti 23, 2026, katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, kukagua hali ya utoaji wa huduma kwa wananchi. Alipowasili hospitalini hapo, Dkt. Mwigulu ametembelea wodi mbalimbali, zikiwemo Wodi ya Mama na Mtoto na Wodi ya Upasuaji, ambako amezungumza na wagonjwa pamoja na ndugu zao na kusikiliza maoni yao kuhusu huduma zinazotolewa hospitalini hapo na changamoto wanazokabiliana nazo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi wanaopata huduma hospitalini hapo wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Serikali kwa ujumla kwa kuendelea kuboresha huduma za afya na mazingira ya utoaji wa huduma hospitalini hapo. Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila; Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Saad Mtambule; pamoja na viongozi wa Hospitali hiyo.

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA MWANANYAMALA

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amefanya ziara ya kushtukiza leo Jumapili, Agosti 23, 2026, katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, kukagua hali ya utoaji wa huduma kwa wananchi. Alipowasili hospitalini hapo, Dkt. Mwigulu ametembelea wodi mbalimbali, zikiwemo Wodi ya Mama na Mtoto na Wodi ya Upasuaji, ambako amezungumza na wagonjwa pamoja na ndugu zao na kusikiliza maoni yao kuhusu huduma zinazotolewa hospitalini hapo na changamoto wanazokabiliana nazo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi wanaopata huduma hospitalini hapo wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Serikali kwa ujumla kwa kuendelea kuboresha huduma za afya na mazingira ya utoaji wa huduma hospitalini hapo. Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila; Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Saad Mtambule; pamoja na viongozi wa Hospitali hiyo.

MSHINDI MAONESHO YA ELIMU,UJUZI NA UBUNIFU KUIWAKILISHA TANZANIA KIMATAIFA

 Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Washindi kupitia maonesho ya Elimu ujuzi na ubunifu yanayoendelea kufanyika kitaifa mkoani Tanga wanatarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika maonesho ya kidunia kwenda kuonesha ujuzi ,ubunifu na maarifa yao. Hayo yameelezwa na katibu mtendaji kutoka baraza la Taifa la elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (NACTVET) Mwajuma Lingwanda wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho hayo ambapo amesema jumla ya washiriki 49 waliopatikana kwenye mchujo uliofanyika katika ngazi ya Kanda watashindanishwa kwenye vipengele 9 ambapo kila mshidi atakata tiketi ya kwenda kuiwakilisha Tanzania kimataifa. "Mashindano haya yalianza katika ngazi ya Kanda ambapo tulikiwa na washiriki katika maeneo 9 ya ujuzi na baada ya hapo tumefikia kwenye maonesho ya kitaifa na tuna washiriki 49 kutoka kwenye taasisi mbalimbali waamuzi wako tayari wale watakaofanikiwa kufaulu na kuwa washindi wa kwanza watapata nafasi ya kushiriki kwenye mashindano ya k...

MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (TEA),KUKUZA NDOTO ZA VIJANA

 Na Mwanamkuu Mwandoro , Tanga. MWANAFUNZI wa amali ya upishi kutoka shule ya Sekondari ya wasichana ya Korogwe iliyopo mkoani Tanga Ntuli Danken Mwanganga ameanza kuona mwanga hadi kutamani kutimiza ndoto ya kuwa mfanyabiashara mkubwa wa chakula ujuzi ambao alianza kujifunza kutoka mikononi mwa Mama yake mzazi aliyekuwa mama ntilie akihitaji kuiboresha zaidi biashara hiyo.  Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya elimu ujuzi na ubunifu yanayoendelea kufanyika kitaifa mkoani Tanga Ntuli ameishukuru mamlaka ya elimu Tanzania (TEA)kwa kuwapatia vifaa ambavyo vimekuwa msaada mkubwa katika kujifunza kwao kwani vimewaongezea uelewa tofauti na awali walipokuwa wakijifunza kwa nadharia pekee. "Mwanzo wakati hatujaletewa vifaa ilikiwa shida sana kujifunza tulikiwa tunasoma tu na kuelekezwa hata matokeo yetu hayakuwa mazuri lakini sasa tunawashukuru sana TEA kwa kutuletea vifaa tunajifunza kwa vitendo na kutumia vifaa" "Nimependa na nimechagua somo la upishi ...

CHATANDA: UTHABITI WA RAIS SAMIA UMEKAMILISHA MRADI WA UMEME WA JNHPP

 NA: MWANDISHI WETU Historia kubwa imeandikwa Tanzania. Hii ni kufuatia kukamilika kwa mradi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP), chenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 katika eneo la mradi, wilayani Rufiji, mkoani Pwani. Kukamilisha kwa mradi huo uliogharimu shilingi trilioni 7.452, kunachochea moja kwa moja maendeleo ya shughuli za kijamii na kiuchumi kupitia uzalishaji wa nishati ya umeme ambayo ni muhimu katika shughuli hizo. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi mradi huo Agosti 22, 2026 wilayani Rufiji.  Akitoa maoni yake kuhusiana na uzinduzi wa mradi huo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Mary Chatanda, amesema kama Rais Dk. Samia asingekuwa thabiti katika uongozi wake, mradi huo usingekamilika. "Rais Dk. Samia alipoingia madarakani mwaka 2021, alikuta mradi huu umefikia utekelezaji wa asilimia 33, lakini ndani ya miaka mitano ya uongozi wake, mradi huo umekamilika wote na unazalisha megawati 2,115 za umeme...

BRELA YAWAHIMIZA WABUNIFU KUSAJILI BUNIFU ZAO MAPEMA KUDHIBITI BIDHAA BANDIA

 Na MASHAKA MHANDO, Tanga WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umesema kuwa hatua ya mbunifu kusajili bidhaa au kazi aliyoibuni ni njia pekee na madhubuti ya kuitofautisha kazi hiyo na bidhaa bandia zinazoweza kuingizwa sokoni na wajanja kwa lengo la kujinufaisha isivyo halali. Wito huo umetolewa na Afisa Usajili kutoka BRELA, Benedickson Willson, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara mkoani Tanga. Willson amesema BRELA imeshiriki katika maonyesho hayo, yanayofanyika kuanzia Agosti 15 hadi 24 mwaka huu, kwa lengo la kuwafikia wabunifu na kuwaelimisha umuhimu wa kusajili kazi zao ili kupata haki ya kipekee ya kuzitumia na kuzilinda dhidi ya matumizi yasiyoidhinishwa. Akifafanua kuhusu ulinzi huo, Afisa huyo alisema kuwa usajili wa alama ya biashara na huduma humwezesha mmiliki kulinda chapa yake, huku akisisitiza kuwa ukiwa umesajili alama yako un...