■ *Waziri Mavunde ataka mnyororo wote wa utoroshaji wa madini hayo udhibitiwe,* ■ *Asikitishwa na upotevu wa mapato ya Serikali yatokanayo na vitendo hivyo,* ■ *Aelekeza wahusika wote wafutiwe leseni na kutoruhusiwa tena kufanya biashara ya madini,* ■ *Atoa rai kwa wananchi kufanya biashara ya madini kupitia mfumo rasmi* 📍Dar es Salaam, Kufuatia kuimarishwa kwa mfumo wa udhibiti wa biashara haramu ya madini unaofanywa na Wizara ya Madini kupitia Kikosi Kazi (Taskforce), madini aina ya dhahabu Gramu 4,402.20 yenye thamani ya 1,238,458,594.42 yamekatwa yakitoroshwa. Hayo yamesemwa leo tarehe 27 Julai, 2026 na Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari. "Serikali kupitia Wizara ya Madini iliunda Kikosi kazi ambacho kinahusisha vyombo vya dola ili kudhibiti biashara haramu ya madini na utoroshaji. Hii ni sehemu tu ya kazi ambazo zimeendelea kufanywa na Kikosi kazi hicho katika kuimarisha mfumo wa ufanyaji biasha...
Marato tv - Sauti ya Jamii