Skip to main content

Posts

Showing posts from August 22, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WASIRA: CCM ITAHAKIKISHA UCHUMI WA TANZANIA UNAENDELEA KUWA IMARA

*Asema lengo ukuaji ufikie asilimia saba ifikapo mwaka 2030* MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema CCM inalenga kuhakikisha uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia saba ifikapo mwaka 2030, huku ukichochea ongezeko la kipato na kuboresha maisha ya wananchi. Wasira amesema hayo leo (Agosti 21,2026) wakati akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa CCM mkoani Singida, akieleza kuwa ukuaji wa uchumi hautakuwa na maana iwapo hautaonekana katika maisha ya mtu mmoja mmoja kupitia ongezeko la kipato na fursa za kiuchumi. Amesema katika Ilani ya CCM, chama hicho kimeweka msisitizo wa kukuza uchumi jumuishi unaolenga kumwezesha kila Mtanzania kunufaika na ukuaji wa uchumi. “Katika Ilani yetu tumesema tunataka uchumi mkuu ambao kila siku mnasikia Tanzania uchumi wako unakuwa kwa asilimia 6.3. Lakini hii haitoshi. Tunataka uchumi huu usaidie maisha ya mtu mmoja mmoja,” amesema Wasira. Ameeleza kuwa CCM inalenga kuona mapato ya wananchi yanaongezek...

ALIYEPOTEA MIAKA 52, AREJEA SONGEA MAMA YAKE HAAMINI ANGUA KILIO

 Na Mashaka Mhando, Tanga Hatimaye, Mzee Mohamed Rashid Mkwaje, ambaye aliondoka nyumbani kwao tangu mwaka 1974 kwenda kufanya kazi ya kukata mkonge wilayani Muheza, amefanikiwa kurejea na kuungana tena na familia yake katika Kijiji cha Ligunga, wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, baada ya kupita miaka 52. Mzee huyo amepokelewa kwa hisia kali na vilio vya furaha, hasa kutoka kwa mama yake mzazi, Asmin Kandulu ambaye alikuwa amekata tamaa na kutokuwa na uhakika kama mwanaye alikuwa bado hai baada ya ukimya wa zaidi ya nusu karne.  Kufuatia mapokezi hayo, wajukuu na ndugu wengine wa familia walimfanyia matambiko maalum ya kimila yaliyoambatana na nyimbo za asili za kabila la Kihiyao, ikiwa ni ishara ya kumpokea na kusherehekea kurejea kwa mtoto wao aliyekuwa amepotea. Safari ya kurejea kwa Mzee Mkwaje ilianza Alhamisi Augosti 20 akitokea Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, ambapo alisindikizwa na Ofisa Ustawi wa Jamii wa wilaya hiyo, Silvanus Misigaro. Akizungumza baada ya kufanikisha sa...

MTAMBI AMPONGEZA GHATI KWA KUWA MTETEZI WA BIMA YA AFYA KWA WOTE MARA

 MKUU wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amempongeza Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Ghati Chomete, kwa dhamira yake ya kuhamasisha wananchi kujiunga na Bima ya Afya kwa Wote, akisema juhudi hizo ni muhimu katika kulinda familia dhidi ya mzigo wa gharama za matibabu. Kanali Mtambi amesema hatua ya Mbunge huyo kuandaa Kongamano la Bima ya Afya kwa Wote ni mfano wa uongozi unaogusa maisha ya wananchi moja kwa moja, kwa kuwa afya ni msingi wa ustawi wa familia na maendeleo ya jamii. Akizungumza katika kongamano hilo, Kanali Mtambi amesema bado kuna wananchi ambao hawajaelewa kikamilifu umuhimu wa kuwa na bima ya afya, hivyo juhudi za viongozi kupeleka elimu kwa wananchi zinapaswa kuungwa mkono. Amesema Bima ya Afya kwa Wote inatoa kinga dhidi ya changamoto ya gharama kubwa za matibabu ambazo zimekuwa zikizikabili familia nyingi, huku akisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kutumia fursa hiyo kuhakikisha wanapata huduma za afya bila mzigo mkubwa wa gharama. “Hongera sana Mheshimiwa...

GHATI CHOMETE AUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA KUFIKISHA BIMA YA AFYA KWA WOTE

 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Mhe. Ghati Chomete, ameunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya kupitia utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, akieleza kuwa Mkoa wa Mara umeendelea kutekeleza kwa vitendo zoezi hilo kwa kuhamasisha wananchi kujiunga na mfumo wa bima ya afya. Akizungumza katika hafla ya Kongamano la Bima ya Afya kwa Wote lililofanyika mkoani Mara, Mhe. Chomete amesema hatua hiyo ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na uhakika wa kupata huduma za afya bila kikwazo cha gharama. Amesema viongozi na wananchi wa Mkoa wa Mara wana wajibu wa kuunga mkono juhudi hizo kwa kuhakikisha wananchi wanaelewa umuhimu wa kuwa na bima ya afya na kutumia fursa hiyo kujiunga na mfumo huo. Mhe. Chomete amempongeza Rais Samia kwa kuweka msukumo mkubwa katika kuboresha sekta ya afya na kusimamia malengo ya kuongeza idadi ya Watanzania wanaonufa...

ZIARA YA MAGANYA ILIVYOTUMIKA KUMPIGISHA "SHOTI" MBUNGE WAITARA TARIME

 MBUNGE wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, amemtupia lawama Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tarime, akidai kuwa uongozi huo uliwatelekeza wajumbe wa chama waliokuja kutoka kata mbalimbali za wilaya hiyo kwa kushindwa kuwaandalia mahitaji muhimu, ikiwemo nauli, chakula na vinywaji. Waitara ametoa kauli hiyo mara baada ya kushiriki kongamano la Bima ya Afya pamoja na changizo la ujenzi wa bweni lililoandaliwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Gati Chomete, akisema alilazimika kusafiri usiku kutoka Dodoma ili kushiriki shughuli hiyo kama sehemu ya kuonesha mshikamano na umoja miongoni mwa wananchi wa Mkoa wa Mara. Amesema alifika katika shughuli hiyo kwa sababu agenda ya ujenzi wa bweni ni muhimu kwa watoto, kwani itawapa mazingira bora ya kujifunza na kujisomea, huku akisisitiza kuwa viongozi wa Mara wanapaswa kushirikiana katika shughuli zenye manufaa kwa wananchi. “Mimi nimetoka Dodoma, nimesafiri usiku usiku kuja hapa kwenye changizo hili kwa sababu kuna agenda muhimu ya ku...

NACTVET: WAPISHI WA WORLDSKILLS WAWE MABALOZI WA UKARIMU AFCON 2027

  Kuelekea fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, washiriki wa fani ya upishi katika Mashindano ya Kitaifa ya Ujuzi WorldSkills Tanzania 2026 wametakiwa kujiandaa kuwa mabalozi wa utalii na ukarimu wa Tanzania kupitia umahiri wao wa kupika. Wito huo umetolewa leo Agosti 22,2026 na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Bi. Bernadetta Ndunguru, alipotembelea mashindano yanayoendelea katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, jijini Tanga. Ndunguru amesema washiriki hao tayari wameonesha kiwango cha juu cha taaluma na wanapaswa kujiona kama wapishi wakubwa watakaokuwa sehemu ya kuipokea Afrika wakati Tanzania itakapokuwa mwenyeji wa AFCON 2027. Kwa mujibu wa Ndunguru, ubora wa huduma za chakula na ukarimu vinatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya taswira ya Tanzania mbele ya maelfu ya wageni kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika. "Niwahimize vijana muendelee kuboresha ujuzi wenu na kutumia fursa ya WorldSkil...

RAIS SAMIA: JNHPP YAKAMILIKA, ATOA AGIZO LA TAHADHARI YA MVUA NA UHIFADHI WA VYANZO VYA MAJI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kila kitu katika Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) kimekamilika na kinafanya kazi, akieleza kuwa kukamilika kwa mradi huo ni fahari kubwa kwa Taifa na uthibitisho kwamba ndoto ya kuwa na mradi mkubwa wa kuzalisha umeme imetimia. Rais Samia amesema hayo leo Agosti 22, 2026, wakati wa hafla ya uzinduzi wa JNHPP iliyofanyika Rufiji mkoani Pwani, ambapo amezindua Kituo cha Kuzalisha Umeme, kutembelea mitambo ya kuzalisha umeme, pamoja na kukagua tuta kuu na kituo cha kupokea na kusafirisha umeme kwenda kwenye Gridi ya Taifa. Amesema Desemba 22, 2022 alifika katika eneo hilo kushuhudia kufungwa kwa njia ya kugeuza maji ya Mto Rufiji na kuanzishwa rasmi kwa ujazaji wa maji katika bwawa, wakati huo ujenzi wa mradi huo ukitarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miaka mitatu. Kwa mujibu wa Rais Samia, kwa neema ya Mungu, bwawa hilo lilijaa ndani ya mwaka mmoja na nusu na kuanza majaribio ya uzalishaji ...