Skip to main content

Posts

Showing posts from September 24, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tume ya Madini Yawakaribisha Wananchi Kutembelea Banda la Geita Gold Fair 2025

  Tume ya Madini kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini inawakaribisha wadau wa madini, wawekezaji, jamii na wananchi kwa ujumla kutembelea banda lake kwenye maonyesho yanayoendelea ya Geita Gold Fair 2025. Maonesho hayo yanayoanza Septemba 18 hadi 28, 2025 yanafanyika katika Viwanja vya Dk Samia Suluhu Hassan Bombambili – Geita. Katika banda hilo, wageni watapata fursa ya kuchunguza fursa mbalimbali za uwekezaji katika mnyororo wa thamani ya madini, ikiwa ni pamoja na utafutaji, uchimbaji madini, usindikaji na biashara. Tume inaonesha uwezo mkubwa ndani ya sekta ya madini nchini Tanzania, huku mkazo ukiwa ni kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kushiriki katika kujenga tasnia endelevu na yenye ushindani. Aidha, banda hilo linaangazia hatua za kimkakati zinazotekelezwa ili kuiweka Tanzania kuwa kitovu cha maendeleo endelevu ya madini na uongezaji thamani. Wageni pia watapata maarifa muhimu kuhusu Miongozo ya Maudhui ya Ndani, ambayo imeundwa ili kuhakiki...

Kigida chaokoa afya na mazingira katika uchenjuaji dhahabu

Geita, Septemba 25, 2025 Tume ya Madini imeendelea kutoa elimu kwa wachimbaji kuhusu matumizi ya Kigida (Retort), kifaa kinachosaidia kulinda afya za wachimbaji, mazingira na kupunguza gharama za matumizi ya zebaki katika uchenjuaji wa dhahabu. Akizungumza kwenye Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili mkoani Geita, Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Hyasinta Rugeiyamu, amesema Kigida kimeundwa kwa mfumo unaozuia mvuke wa zebaki kuingia mwilini wakati wa uchenjuaji, hivyo kumlinda mchenjuaji dhidi ya madhara ya kiafya. “Mbali na kulinda afya, Kigida huzuia pia moshi wa zebaki kutawanyika hewani. Badala yake, mvuke huo hubadilishwa kuwa kimiminika kinachohifadhiwa na kutumika tena. Hii husaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira na gharama za ununuzi wa zebaki mpya,” amefafanua Rugeiyamu. Ameongeza kuwa Tume ya Madini itaendelea kuhamasisha wachimbaji kote nchini k...

DC Kingalame Apongeza TBA kwa Wazo la Mradi Mkubwa wa Makazi ya Biashara Geita

Geita – Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Grace Kingalame, ameipongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kuja na wazo la kuanzisha mradi mkubwa wa Makazi ya Biashara mkoani Geita, akisema hatua hiyo ni tafsiri ya maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha Watanzania wanapata makazi bora. Akizungumza mara baada ya kutembelea maonyesho ya nane ya teknolojia ya madini yanayoendelea katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili mkoani Geita, Kingalame alisema mradi huo ni fursa muhimu ya maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla  “Makazi haya yataleta raha kwa sababu watumishi na wananchi kwa ujumla watapata makazi bora ya kuishi. Hii ndiyo tafsiri ya Rais Dkt. Samia anatamani watu wake wakae kwenye maeneo mazuri,” alisema Kingalame. Aidha, amewapongeza TBA kwa uamuzi wa kukaribisha sekta binafsi kushirikiana nao katika utekelezaji wa mradi huo, akisema ushirikiano huo utasaidia kukamilisha makazi hayo kwa muda muafaka.  “Naita...

Ujenzi wa barabara za lami kukuza uchumi wa wananchi Tanganyika

Tanganyika - Katavi Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2025 Ndugu Ismail Ali Ussi, ameipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Mkoa wa Katavi kwa kutekeleza ujenzi wa barabara za kiwango cha lami za Mji wa Majalila Wilaya ya Tanganyika Mkoani humo zenye urefu wa km 4.0 huku zikitajwa kuwa chachu ya ustawi wa maendeleo ya watu  kiuchumi na Kijamii. Ussi amezungumza hayo mara baada ya kuzindua barabara hizo na kuongeza kuwa utekelezaji makini wa majukumu ya TARURA  utawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi kutokana na unafuu utakaokuwepo kutokana na kuimarika kwa miundombinu ya usafirishaji  hivyo kila mmoja atanufaika na ukuaji wa uchumi. Awali akisoma taarifa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 Ismail Ali Ussi, Meneja wa TARURA Wilaya ya Tanganyika Mhandisi. Nolasco Kamasho amesema mradi  wa barabara  za Mji wa Majalila uliojengwa Kijiji cha Majalila Kata ya Tongwe una urefu wa km 4.0 na umegharimu zaidi ya...

Wasira:Miaka Mitano Ijayo Tanga itamelemeta

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira amewahakikishia wananchi wa Pangani kwamba miaka mitano ijayo katika utekelezaji wa Ilani yake ya Uchaguzi ya 2025-2030 itabeba neema kubwa kwa maendeleo ya wilaya hiyo. Miongoni mwa neema hizo ni pamoja na kukamilika kwa barabara ya Tanga-Pangani-Bagamoyo kupitia Saadani ambayo itafungua uchumi wa wilaya hiyo na mkoa wa Tanga kwa ujumla. Wasira aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wana CCM waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wa ndani wa Chama uliowashirikisha viongozi wa wilaya hiyo na mkoa wa Tanga kwa ujumla. Alisema mbali na barabara, pia miaka mitano ijayo iwapo CCM itachaguliwa kurudi madarakani serikali yake itaongeza shule za msingi, sekondari, zahanati na vituo vya afya. Aidha, Wasira amewapokea wanachama wapya 153 waliohamia CCM kutoka vyama mbalimbali vya siasa akiwemo Katibu wa ACT Wazalendo... Awali, Wasira amesema kazi kubwa iliyopo mbele ya wana CCM ni kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kupiga kura na kuwashawi...

*Serikali yaondoa Vat Kwa Vituo vya Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (Cng)

📌 *Lengo ni kuongeza uwanda wa  matumizi ya CNG katika vyombo vya moto nchini* 📌 *Mhandisi Mramba azindua kituo cha Gesi Asilia iliyoshindiliwa ( CNG) cha PUMA Energy* 📌 *Asema vifaa vya kuwekea mifumo  ya gesi  kwenye vyombo vya moto pia imeondolewa* 📌 *Apongeza PUMA Energy kwa kuiunga mkono Serikali katika ujenzi wa vituo vya CNG* Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba amesema  Serikali imeondoa kodi ya ongezeko la thamani  (VAT) kwa vituo vyote vya Gesi iliyoshindiliwa (CNG) nchini  ili kuhamasisha matumizi ya gesi asilia  kwenye vyombo vya moto kupitia uwepo wa vituo vingi vya kutoa huduma hiyo kwa wananchi.  Amesema kuwa Serikali pia imeondoa kodi kwenye vifaa vya kuwekea mifumo hiyo ya gesi  kwenye vyombo vya moto kama vile magari na bajaji ikiwa ni hatua pia ya kuhamasisha matumizi ya gesi asilia katika vyombo vya moto. Mhandisi Mramba ameeleza hayo leo Septemba 24, 2025 jijini Dar es Salaam wakati  akizindua ...

Peter Zakaria Ateuliwa Chifu wa 7 Kabila la Kurya Koo ya Butimbaru

Mdau wa maendeleo mkoa wa mara na kada wa chama cha mapinduzi (CCM) Ndg. Peter Zakaria leo Tarehe 24 September 2025 amepokea wito wa kufika katika kilinge/baraza/eneo wanapokalia wazee wa mila ya koo ya Butimbaru Inchage linaloitwa "Kungurutani" linalopatikana katika kijiji cha mogabiri ikiwa ndio eneo linalotumika kutatua migogoro inayofikishwa na jamii ya kurya ndani ya hilo la mila. Zakaria alifika na kupashwa habari ya Uteuzi wa jina lake kupendekezwa kati ya majina mengi na kuibuka kidedea kuwa chief wa koo hiyo. Akizungumza katika kikao hicho cha mila mwenyekiti wa mila koo ya butimbaru na mjumbe wa koo 12 Ndg.Charles Mwita Mgogo amesema wazee wamemteua kuwa chifu wao baada ya kufanyika kwa vikao mbalimbali vya majadiliano na wito huo wa leo kwa Zakaria ni kwaajili ya kupashwa habari hiyo ili kujua utayari wake. "Hapa tulipo ndio makao yetu tunapokalia kwaajili ya kutatua migogoro ya wananchi pamoja na kumsikiliza shida zao mbalimbali. Leo imekuwa ni siku nzuri na ...

Tume ya Madini yavunja rekodi ya upimaji sampuli kwa mwaka 2024/2025

Maabara ya Tume ya Madini imevuka lengo la upimaji sampuli za madini kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 30, 2024/2025, baada ya kupima jumla ya sampuli 7684 dhidi ya lengo la 6,800.  Hili ni ongezeko linaloashiria ufanisi mkubwa wa maabara katika kutoa huduma kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini. Akizungumza katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita, Mkemia  kutoka maabara hiyo, David Lyandala amesema maabara inaendelea kutoa huduma za kitaalam za uchunguzi wa madini ili kubaini ubora na kiasi kilichomo.  Huduma hizo zinajumuisha uchunguzi wa dhahabu, makinikia, kaboni, kimiminika chenye dhahabu, mbale za udongo na miamba kwa kutumia (Fire Assay), pamoja na uchunguzi wa metali kama shaba, chuma, nikeli, manganizi, galena na zinki kwa kutumia mashine za kisasa za X-Ray Fluorescence (XRF). Aidha, maabara hupima madini ya kinywe (graphite), unyevunyevu wa udongo na miamba, pamoja na upotevu wa uzito kwa kuchoma (Loss in Ignition).  Lya...

Dk.Nchimbi Atua Mufindi Kuomba Kura Za Dk Samia …wananchi Wamuahidi Ushindi

Na Mwandishi Wetu.  MGOMBEA mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi ameendelea kufanya mikutano ya kampeni kuelekea Uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu ambapo leo amehutubia maelfu ya wananchi Jimbo la Mufindi mkoani Iringa. Dk.Nchimbi amefanya mkutano wa kwanza wa hadhara wa kampeni katika kata ya Ifwagi,ndani ya Jimbo la Mufindi Kaskazini mkoa wa Iringa baada ya kuhitimisha mikutano yake ya kampeni mkoani Njombe. Akiwa katika mkutano huo amenadi sera na Ilani ya CCM ya mwaka 2025 - 2030 sambamba na kusaka kura za  ushindi wa kishindo za Mgombea urais wa chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani. Pia Dkt.Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kumnadi mgombea Ubunge wa jimbo la  Mufindi Kaskazini  Exaud Kigahe,Wagombea Ubunge wa mkoa huo pamoja na Madiwani. Kwa upande wao wa wananchi wa Jimbo hilo wamemuahidi Dk.Nchimbi kwamba katika Uchaguzi mkuu watapiga  kura za ushindi wa kshindo kwa ...