MBUNGE wa Jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya, ameendelea kusaidia shughuli za dini baada ya kutoa Qur’an, Juzuu na vitabu mbalimbali vya dini ya Kiislamu kwa ajili ya misikiti na waumini wa jimbo hilo. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Katibu wa Mbunge huyo, Mussa Hussein, amesema msaada huo umetolewa kwa lengo la kutatua changamoto ya upungufu wa Qur’an na vitabu vya dini katika misikiti ya Bunda Mjini. Amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za mbunge huyo za kuimarisha nyumba za ibada na kusaidia waumini kupata nyenzo muhimu za kujifunzia dini. “Mheshimiwa Esther Bulaya amekuwa akitoa misaada mbalimbali katika misikiti ya jimbo letu na ataendelea kufanya hivyo. Mbali na msaada huu wa vitabu, pia kuna mipango mingine ya kuendelea kuboresha na kuimarisha nyumba za ibada pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili,” Amesema Kwa upande wake, Sheikh wa kata ya Bunda stoo na Masjid Nuru Seif Haruna Musa Omar Kayege amepokea msaada huo kwa niaba ya waumini na kueleza k...
Marato tv - Sauti ya Jamii