Na Mwandishi wetu Jovina Massano BAADHI ya wazazi na walezi Manispaa ya Musoma wahamasika watoto wao kupata chanjo ya polio awamu ya tatu inayotarajia kuanza Agosti 27,2026. Maria Kimario mkazi wa mtaa wa Sokoine Kata ya Mukendo amewapongeza waratibu, wahamasishaji na vyombo vya habari kwa kuweza kutoa taarifa kwa wakati. Amesema wahamasishaji na viongozi wa mitaa wameweza kuwafikia na kuwapa elimu ya umuhimu wa chanjo hiyo lakini pia taarifa ya chanjo hiyo inaonekana kwenye vyombo vya habari. "Elimu na taarifa zinapotolewa mapema husaidia wazazi na walezi kujiandaa na kuitikia kwa wingi na kuwaepusha watoto kupooza kwa ghafla"amesema Maria. Pia ameiomba viongozi kuwa na utaratibu wa kutoa elimu za masuala mbalimbali yanayoihusu Jamii ili kuondoa migongano isiyo ya lazima. Eliza Sryvesta mkazi wa Mtakuja B kata ya Mwisenge amesema kuwa chanjo hii ni Muhimu kwa kuwa hivi sasa imepunguza magonjwa ya polio,ulemavu kwa watoto. Ameongeza kuwa watoto wenye ulemavu miaka ya ...
Marato tv - Sauti ya Jamii