Skip to main content

Posts

Showing posts from June 10, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

AJIRA KIPAUMBELE KATIKA UTEKELEZAJI WA DIRA 2050

Serikali imeeleza dhamira yake ya kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania kupitia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, huku uzalishaji wa ajira ukipewa nafasi ya kipekee katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2026/27. Akiwasilisha mpango huo bungeni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema mpango huo umeandaliwa kwa lengo la kugeuza maono ya Dira 2050 kuwa miradi na programu zenye matokeo ya moja kwa moja kwa wananchi, hususan katika kukuza uchumi na kuzalisha ajira. Mpango wa mwaka 2026/27 ni mwanzo wa utekelezaji wa Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2026/27–2030/31), unaobeba dhima ya "Mageuzi kwa Ajili ya Ukuaji Jumuishi wa Uchumi na Uzalishaji Ajira." Katika kufanikisha lengo hilo, serikali imeelekeza nguvu katika sekta zenye mchango mkubwa wa ajira ikiwemo kilimo, viwanda, madini, utalii, biashara pamoja na huduma za teknolojia na ubunifu, ambazo zinatajwa kuwa nguzo muhimu za kukuza uchumi na k...

SERIKALI YATOA MWELEKEO KUKABILIANA NA UHABA WA MAJOSHO BUTIAMA

 Serikali imesema itaendelea kushughulikia changamoto ya uhaba wa majosho katika Jimbo la Butiama, huku ikizitaka halmashauri nchini kutumia ipasavyo mapato yatokanayo na mifugo ili kuboresha huduma za afya ya mifugo kupitia ujenzi na ukarabati wa majosho. Akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Butiama, Dkt. Charles Mahera, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, amesema Serikali inatambua mahitaji yaliyopo katika jimbo hilo na tayari imepokea barua rasmi iliyowasilishwa na mbunge huyo, ambayo itasaidia kutoa mwongozo katika utekelezaji wa vipaumbele vya sekta ya mifugo.  Waziri Kakurwa amempongeza Dkt. Mahera kwa kuibua na kufuatilia suala hilo kwa njia rasmi, akibainisha kuwa ushirikiano kati ya Serikali, wabunge na mamlaka za serikali za mitaa ni muhimu katika kutatua changamoto zinazowakabili wafugaji. Amesisitiza kuwa majosho yana mchango mkubwa katika kudhibiti magonjwa ya mifugo, kuboresha afya ya wanyama na kuongeza uzalishaji, hivyo ni muhimu kw...

CHATANDA: SINGAPORE IMEJIRIDHISHA NA MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI YALIYOPO TANZANIA

 NA: MWANDISHI WETU, DODOMA Tanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara ambayo yanawavutia viongozi, wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kuwekeza na kuchangia ukuaji wa maendeleo na uchumi. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa (MCC), Mary Chatanda Juni 10, 2026, Jijini Dodoma, kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Singapore, Tharman Shanmugaratnam nchini. "Ujio wa Rais wa Singapopre nchini ni kielekezo cha kuimarika kwa diplomasia nchini. Lakini tukumbuke pia ujio wake ni wa kimkakati, kuhakikisha Singapore na Tanzania zinashirikiana katika maeneo mbalimbali ya kimaendeleo. Wenzetu wa Singapore wamejiridhisha pasi na shaka juu ya mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo Tanzania,"amesema Chatanda. Sanjari na hilo, Chatanda amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya maboresho makubwa ya mazingira ya uwekezaji na biashara ambapo wawekezaji wameongezeka. "Kila mwen...

RAIS DKT. MWINYI AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA SINGAPORE KUTUMIA FURSA ZA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuimarisha mazingira bora ya uwekezaji, uwazi na sera rafiki ili kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha uwekezaji kinachotambulika katika ukanda wa Afrika Mashariki. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 10 Juni 2026, aliposhiriki dhifa maalum ya Singapore–Zanzibar Business Networking Dinner iliyofanyika Fumba, Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Singapore kutumia fursa zilizopo Zanzibar katika sekta za utalii, uchumi wa buluu, biashara, teknolojia, huduma na miundombinu. Amesema ziara ya Rais wa Singapore, Mhe. Tharman Shanmugaratnam, pamoja na Jukwaa la Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Zanzibar na Singapore, zimefungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kiuchumi na uwekezaji kati ya pande hizo mbili. Katika hafla hiyo, Rais Dkt. Mwinyi ametunukiwa Tuzo Maalum ya Uongozi katika Uwekezaji na Shirikisho la Waweke...

ZAIDI YA WAKULIMA 200 WA ZAO LA PAMBA WAFUNGUA AKAUNTI IGUNGA

  Zaidi ya wakulima 200 wa zao la pamba kutoka vijiji vya Mwahalanga, Bukama, Mwabakima, Jogoya na Jilelabalimi vilivyopo katika Wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora, wamefungua akaunti za benki na kusajili laini za simu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kupokea malipo ya mazao yao kwa njia ya kidijitali, hatua inayolenga kuongeza uwazi, usalama na uharaka wa malipo. Wakulima hao wamefungua akaunti kupitia Benki ya NMB pamoja na kusajili laini kupitia Mtandao wa simu wa Mixx by Yas, hatua ambayo itawawezesha kupokea fedha zao kwa urahisi kupitia mifumo ya benki na simu za mkononi. Ufunguzi wa akaunti hizo na usajili wa laini za simu unatekelezwa kufuatia maelekezo ya waraka wa Mrajis wa Vyama vya Ushirika unaozitaka AMCOS za wakulima wa pamba kuhakikisha malipo ya wakulima yanafanyika kupitia akaunti za benki na huduma za fedha kwa njia ya simu, badala ya kutumia mfumo wa malipo ya fedha taslimu (cash). Lengo la hatua hiyo ni kuongeza uwazi, usalama wa fedha za wakulima, kurahisisha ufu...

SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI – DKT. MWIGULU

Ahimiza kuwekeza kwenye miundombinu inayochochea vyanzo vya uwekezaji._ WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kuondoa vikwazo na kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi ili kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini. Ameyasema hayo leo (Jumatano, Juni 10, 2026), wakati akizindua ghala la forodha la kampuni ya Ciwaye Trading Co. Ltd Wilayani Chamwino mkoani Dodoma. “Kama tunavyoheshimu sekta ya umma, tunatakiwa kuheshimu sekta binafsi kwa uzito ule ule, kama mataifa mengine yaliyoendelea, uchumi wa mataifa hayo nguzo yake ni sekta binafsi.” Dkt. Mwigulu aliongeza kwa kusema “Kwa kuheshimu hilo, nimeona nije kuzindua mradi huu, kama ambavyo nimepita kwenye ziara kuzindua miradi ya Serikali, ndiyo maana nimeona na hapa nije mwenyewe.” Aidha, ameeleza kuwa mradi huo una umuhimu mkubwa katika maendeleo ya nchi, hivyo hauna budi kulelewa. “Ukubwa wa jambo hili haupimwi kwa majengo, bali kwa uthubutu na matokeo yanayoakisi Dira yetu ya maendeleo na maono ya Rais wetu ya ku...

MKUU WA JESHI LA MAGEREZA AFUNGUA MAFUNZO YA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA UREKEBISHAJI KWA MAAFISA USTAWI WA JAMII

 Na. Ssgt Mawazo Mtondo - Dodoma. Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, leo Juni 10, 2026, amefungua rasmi Mafunzo kwa Maafisa Ustawi wa Jamii kuhusu Mwongozo wa Utekelezaji wa Programu za Urekebishaji katika Ukumbi wa Rugimbana, Msalato, jijini Dodoma. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, CGP Katungu aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kwa namna inavyoendelea kuliwezesha Jeshi la Magereza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Alisema Serikali imekuwa ikitoa rasilimali fedha kwa ajili ya  ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya magereza, makazi ya watumishi, vyombo vya usafiri pamoja na kugharamia mafunzo mbalimbali kwa watumishi wa Jeshi la Magereza. CGP Katungu alibainisha kuwa moja ya majukumu ya msingi ya Jeshi la Magereza ni urekebishaji wa wafungwa kwa kuwapatia elimu, ujuzi na maarifa ili wanapomaliza vifungo vyao warejee katika j...