Skip to main content

Posts

Showing posts from June 16, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wasira Aeleza Sababu za Ccm,Kuhitajika Milelele

Na Mwandishi Wetu MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira ameeleza mambo mbalimbali yanayoifanya CCM kuwa idumu. Mojawapo ya sababu hizo ni wajibu wake wa majukumu endelevu ya kuwatumikia Watanzania. Amesema kutokana na umuhimu wa majukumu hayo kwa ustawi wa nchi na maisha ya Watanzania CCM itakuwepo wakati wote. Wasira ameyasema hayo leo Juni, 16, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita ambako ameanza ziara ya siku tatu ya kukagua uhai wa Chama, kuzungumza na wana CCM na makundi mbalimbali yakiwemo ya viongozi wa dini, wakulima na wafugaji. "CCM ni Chama kikubwa na chenye historia, watu wengi wanadhani CCM ilianza miaka 48 iliyopita, Chama hiki kimerithi mikoba ya vyama vya TANU na Afro Shiraz Party. TANU ina miaka 75 na Afro Shirazi Part y miaka 67. "CCM ni Chama kipya ambacho kimeundwa na vyama vya zamani. Kimekabidhiwa majukumu ya kudumu, hivyo tukisema kidumu Chama Cha Mapinduzi hatuna utani. Tun...

Kampuni Kubwa za Madini Zasaini Mkataba Wa Kuuzia Dhahabu Benki Kuu Tanzania(Bot)

▪️Rais Samia apongezwa kwa maono ▪️Kampuni za GGM,Shanta na Buckreef kuuza Dhahabu kwa BOT,GGR kusafirisha dhahabu. ▪️BOT yanunua Tani 5 ya dhahabu  ▪️Waziri Mavunde apongezwa kwa usimamizi mzuri wa Sekta ya Madini ▪️Tanzania kuingia 10 bora kwa nchi zenye hifadhi kubwa ya Dhahabu Afrika Dodoma Benki ya Tanzania(BOT) leo imesaini mikataba na Kampuni za Uchimbaji Madini za Geita Gold Mine(GGM),Buckreef Gold Ltd na Shanta Ltd juu kampuni hizo kuiuzia BOT kiasi kisichopungua asilimia 20 ya dhahabu inayozalishwa kama ambayo imeelezwa kwenye kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini,Sura ya 123. Hafla hiyo ya utiaji saini mikataba ya uuzwaji wa dhahabu imefanyika leo tarehe 16.06.2025 Jijini Dodoma na kushuhudiwa na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu L. Nchemba na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde. Akizungumza katika hafla hiyo Mh.Mwigulu Nchemba amempongeza Mh. Rais Dkt. SamiaS. Hassan kwa uongozi wenye maono na ambao umechochea kukua kwa hifadhi ya dhahabu ya BOT hali ambayo itasaidia kuimaris...

Rea Kuendelea Kuwezesha Waendelezaji wa Miradi ya Nishati Vijijini

📌RC Njombe apongeza usimamizi wa miradi ya REA Wakala wa Nishati Vijijini (REA) utaendelea kutoa sapoti kwa waendelezaji wa miradi ya kuzalisha na kusambaza umeme kote nchini ili kuwezesha wananchi wengi kufikiwa na huduma bora ya nishati ambayo inachangia kuinua uchumi wa wananchi pamoja na huduma za  kijamii.  Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu amebainisha hayo Mkoani Njombe Juni 17, 2025 kwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Anthony Mtaka alipofika ofisini kwake kuelezea ziara yake ya kukagua miradi ya kuzalisha na kusambaza umeme mkoani humo.  "Njombe ni moja ya Mkoa ambayo imepokea sapoti kubwa kwenye uendelezaji wa miradi ya nishati jadidifu," alisema Mhe. Balozi Kingu. Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Mtaka alimueleza Mhe. Balozi Kingu namna ambavyo anafarijika kwa sapoti inayotolewa na REA kwenye miradi hiyo na alisema kwa namna mkoa huo ulivyo bado zipo fursa nyingi za kuzalisha umeme kwa maporomoko ya maji ya mito. "Jio...

TFS yakabidhi madawati 100 kwa shule ya sekondari Mvomero, yasaidia kuinua elimu

  Na Mwandishi Wetu, Morogoro Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umekabidhi msaada wa madawati 100 yenye thamani ya Sh8 milioni kwa Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Sokoine, wilayani Mvomero mkoani Morogoro, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa wajibu wa taasisi hiyo kwa jamii. Msaada huo umetolewa kupitia Shamba la Miti la Mtibwa na kupokelewa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Judith Nguli, ambaye amesema hatua hiyo ni mchango muhimu katika kuboresha mazingira ya ujifunzaji kwa wanafunzi. “Tunapongeza hatua hii ya TFS kwa kuonesha mfano bora wa uwajibikaji kwa jamii. Tunatoa wito kwa taasisi nyingine kuiga mfano huu ili kwa pamoja tuweze kuboresha sekta ya elimu na huduma nyingine muhimu kwa wananchi,” alisema DC Nguli wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano. Alitumia nafasi hiyo pia kutoa rai kwa wananchi wa Mvomero kutunza mazingira na rasilimali za misitu kwa kuwa ni sehemu ya urithi wa maendeleo endelevu kwa vizazi vijavyo. Kwa upande wake, Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Mit...

Global Education Link kusafirisha zaidi ya wanafunzi 200 nje ya nchi

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya wanafunzi 200 wanatarajiwa kusafiri kwenda masomoni kwenye mataifa mbalimbali kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026 hivi karibuni kuanza pitia uratibu wa Global Education Link  (GEL). Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa GEL, Abdulmalick Mollel, wakati wa kikao baina ya wanafunzi hao na wazazi wao kuhusu kukamilisha taratibu za safari. Wanafunzi hao wanatarajiwa kusafiri kwenda masomoni kwa nchi za Uingereza, Canada, Marekani Malaysia, Poland, Uturuki na India. Kikao hicho kilifanyika ofisini hapo ambacho kililenga kuwaelimisha wanafunzi hao taratibu na kanuni wanazotakiwa kufuata wanapokuwa masomoni nje ya nchi zikiwemo mila, tamaduni na desturi za nchi wanazotarajia kwenda. “Ni jukumu la GEL kuhakikisha maandalizi yote ya visa na nyaraka zingine zimekamilika na kuhakikisha wanafunzi ambao wameniamini na wazazi wao kuwaelekeza vizuri na jukumu la mwanafunzi ni kusema kozi anayokwenda kusoma,” alisema “Mwanafunzi atasema anataka kozi gani anataka ...

Wafugaji Wamkabidhi Rais Samia Tuzo ya Heshima

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya heshima na shukrani kutoka kwa Mwenyekiti wa wafugaji Ndugu Mrida Mshote mara baada ya kuzindua Mpango wa Miaka Mitano wa Chanjo na Utambuzi wa Mifugo katika viwanja vya Nanenane Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Mpango wa Chanjo na Utambuzi wa Mifugo kitaifa kwa mwaka 2024/2025- 2028-2029 katika viwanja vya Nanenane Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.