MAKAMU WA RAIS AHITIMISHA ZIARA YA SIKU SABA AKIWA KIBITI, ONYO KWA WANAOCHEZEA FEDHA ZA UMMA LATOLEWA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, ametumia salamu zake kwa wananchi wa Kibiti kutoa msukumo wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo, akitaka ahadi ya shilingi milioni 500 za kushughulikia upungufu wa maji ifuatiliwe, huku akionya kuwa watakaochezea fedha za wananchi watachukuliwa hatua. Makamu wa Rais amesema maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha fedha zinazotolewa zinawahudumia wananchi, na kwamba wasaidizi wake wana wajibu wa kusimamia matokeo. “ Mhe. Rais Hataki kuona fedha ya umma inachezewa,” amesema, akisisitiza kuwa Serikali haitamvumilia mzembe wala mtu atakayezichukulia fedha za maendeleo ya Kibiti kuwa mali yake. Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso kuwa Kibiti mjini inakabiliwa na upungufu wa maji wa takribani lita milioni 1.8 kwa siku, na kuahidi Wizara yake kuleta timu ya wataalamu na shilingi milioni 500 kuanza kazi ya kuongeza upatikanaji wa huduma hiyo. Aweso ameeleza kuwa vyanzo mb...