Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo ameupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Annamringi Macha katika Uwanja wa Shule ya Msingi Balili, Halmashauri ya Mji wa Bunda. Akitoa taarifa kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Wazo Michael Mwang'onda Mhe. Mtambi amesema ukiwa katika Mkoa wa Mara Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika kilomita 996 na utatembelea miradi ya maendeleo 63 yenye thamani ya shilingi bilioni 174. Aidha, Mhe. Mtambi amewakaribisha wananchi wa Mkoa wa Mara na maeneo jirani kushiriki katika hafla ya Mwenge wa Uhuru kuwasha Mwenge wa Mwitongo itakayofanyika tarehe 02 Agosti, 2026 Nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwitongo Butiama. Leo Mwenge wa Uhuru unakimbizwa katika Halmashauri ya Mji wa Bunda na baadae katika Halmashauri zote za Mkoa wa Mara hadi tarehe 09 Agosti, 2026 na tarehe 10 Agosti, 2026 utakabidhiwa Mkoa wa Mwanza kuendelea na mbio zake. Kauli mbiu ya...
Marato tv - Sauti ya Jamii