WAZIRI MKUU ATOA MAELEKEZO UENDESHAJI MRADI WA SGR *_Ataka huduma ziboreshwe na usimamizi wa miundombinu uimarishwe_* WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Uchukuzi iendelee kulisimamia kwa karibu Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kuhakikisha huduma za treni ya SGR zinaboreshwa na miundombinu inaimarishwa ili mradi huo uweze kudumu kwa muda mrefu Amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali itaendeleza sekta ya uchukuzi ambapo pamoja na mambo mengine itasimamia sekta ya reli ikiwemo ujenzi wa SGR na uendeshaji wa treni ya kisasa ya abiria kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa tarehe 31 Desemba, 2023 Mheshimwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alielekeza kuanza uendeshaji wa reli ya SGR kwa kipande cha Dar es Salaam - Dodoma ifikapo mwezi Julai, 2024. Ameyasema hayo leo (Septemba 6, 2024) wakati wa kuahirisha Mkutano wa 16 wa Bunge, jijini Dodoma. “Naomba kulitaarifu Bunge lako tukufu kuwa, safari za treni ya mwendokasi kutoka Dar es Salaam...
Marato tv - Sauti ya Jamii